Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

1 Nyakati 1:12-32

1 Nyakati 1:12-32 NEN

Wapathrusi, Wakasluhi (hao ndio asili ya Wafilisti) na Wakaftori. Wana wa Kanaani walikuwa: Sidoni, mzaliwa wake wa kwanza, na Hethi, Wayebusi, Waamori, Wagirgashi, Wahivi, Waariki, Wasini, Waarvadi, Wasemari na Wahamathi. Wana wa Shemu walikuwa: Elamu, Ashuru, Arfaksadi, Ludi na Aramu. Wana wa Aramu walikuwa: Usi, Huli, Getheri na Mesheki. Arfaksadi akamzaa Shela, Shela akamzaa Eberi. Eberi alipata wana wawili: Mmoja wao aliitwa Pelegi, kwa kuwa wakati wake dunia iligawanyika; nduguye aliitwa Yoktani. Wana wa Yoktani walikuwa: Almodadi, Shelefu, Hasarmawethi, Yera, Hadoramu, Uzali, Dikla, Obali, Abimaeli, Sheba, Ofiri, Havila na Yobabu. Wote hawa walikuwa wana wa Yoktani. Wana wa Shemu walikuwa Arfaksadi, Shela, Eberi, Pelegi, Reu, Serugi, Nahori, Tera, Tera akamzaa Abramu (yaani, Abrahamu). Abrahamu alikuwa na wana wawili: Isaki na Ishmaeli. Hawa ndio waliokuwa wazao wa Hagari: Nebayothi mzaliwa wa kwanza wa Ishmaeli, Kedari, Adbeeli, Mibsamu, Mishma, Duma, Masa, Hadadi, Tema, Yeturi, Nafishi na Kedema. Hao ndio wana wa Ishmaeli. Wana waliozaliwa na Ketura suria wa Abrahamu walikuwa: Zimrani, Yokshani, Medani, Midiani, Ishbaki na Shua. Wana wa Yokshani walikuwa: Sheba na Dedani.

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha