1 Mambo ya Nyakati 1:12-32
1 Mambo ya Nyakati 1:12-32 Biblia Habari Njema (BHN)
Wapathrusi Wakaftori na Wakasluhi (hao ndio asili ya Wafilisti). Wana wa Kanaani walikuwa Sidoni, mzaliwa wake wa kwanza, na Hethi. Kanaani pia ndiye babu yao Wayebusi, Waamori, Wagirgashi, Wahivi, Waarki, Wasini, Waarvadi, Wasemari na Wahamathi. Wana wa Shemu walikuwa Elamu, Ashuri, Arpaksadi, Ludi, Aramu, Usi, Huli, Getheri na Mesheki. Arpaksadi alimzaa Shela, Shela akamzaa Eberi. Eberi alikuwa na wana wawili; mmoja wao aliitwa Pelegi, (kwa maana wakati wake watu walikuwa wametawanyika duniani), na ndugu yake aliitwa Yoktani. Wana wa Yoktani walikuwa Almodadi, Shelefu, Hasarmawethi, Yera, Hadoramu, Uzali, Dikla, Obali, Abimaeli, Sheba, Ofiri, Havila na Yobabu. Hao watu ni wana wa Yoktani. Ukoo wa Abrahamu kutokea Shemu ni kama ifuatavyo: Shemu alimzaa Arpaksadi, naye Arpaksadi akamzaa Shela. Shela akamzaa Eberi, Eberi akamzaa Pelegi, Pelegi akamzaa Reu; Reu akamzaa Serugi, Serugi akamzaa Nahori, Nahori akamzaa Tera, na Tera akamzaa Abramu, ambaye ndiye Abrahamu. Abrahamu alikuwa na watoto wawili wa kiume: Isaka na Ishmaeli. Hivi ndivyo vizazi vyao: Mzaliwa wa kwanza wa Ishmaeli alikuwa Nebayothi na wengine ni Kedari, Adbeeli, Mibsamu, Mishma, Duma, Masa, Hadadi, Tema, Yeturi, Nafishi na Kedema. Hao ndio wana wa Ishmaeli. Abrahamu alikuwa na suria aliyeitwa Ketura. Ketura alimzalia Abrahamu: Zimrani, Yokshani, Medani, Midiani, Ishbaki na Shua. Wana wa Yokshani walikuwa Sheba na Dedani.
1 Mambo ya Nyakati 1:12-32 Swahili Revised Union Version (SRUV)
na Wapathrusi, na Wakasluhi; huko ndiko walikotoka Wafilisti, na Wakaftori. Na Kanaani akamzaa Sidoni, mwanawe wa kwanza, na Hethi; na Myebusi, na Mwamori, na Mgirgashi; na Mhivi, na Mwarki, na Msini; na Mwarvadi, na Msemari, na Mhamathi. Wana wa Shemu; Elamu, na Ashuru, na Arfaksadi, na Ludi, na Aramu, na Usi, na Huli, na Getheri, na Mashi. Na Arfaksadi akamzaa Sala, na Sala akamzaa Eberi. Na Eberi akazaliwa wana wawili wa kiume; jina la wa kwanza aliitwa Pelegi, maana katika siku zake nchi iligawanyika; na jina la nduguye aliitwa Yoktani. Na Yoktani akamzaa Almodadi, na Shelefu, na Hasarmawethi, na Yera; na Hadoramu, na Uzali, na Dikla; na Obali, na Abimaeli, na Sheba; na Ofiri, na Havila, na Yobabu. Hao wote ndio wana wa Yoktani. Shemu, na Arfaksadi, na Sala; na Eberi, na Pelegi, na Reu; na Serugi, na Nahori, na Tera; na Abramu, naye ndiye Abrahamu. Wana wa Abrahamu; Isaka, na Ishmaeli. Hivi ndivyo vizazi vyao; mzaliwa wa kwanza wa Ishmaeli, Nebayothi; kisha Kedari, na Abdeeli, na Mibsamu; na Mishma, na Duma, na Masa, na Hadadi, na Tema; na Yeturi, na, Nafishi, na Kedema. Hao ndio wana wa Ishmaeli. Na wana wa Ketura, suria yake Abrahamu; yeye akamzaa Zimrani, na Yokshani, na Medani, na Midiani, na Ishbaki, na Shua. Na wana wa Yokshani; Sheba na Dedani.
1 Mambo ya Nyakati 1:12-32 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
na Wapathrusi, na Wakasluhi; huko ndiko walikotoka Wafilisti, na Wakaftori. Na Kanaani akamzaa Sidoni, mwanawe wa kwanza, na Hethi; na Myebusi, na Mwamori, na Mgirgashi; na Mhivi, na Mwarki, na Msini; na Mwarvadi, na Msemari, na Mhamathi. Wana wa Shemu; Elamu, na Ashuru, na Arfaksadi, na Ludi, na Aramu, na Usi, na Huli, na Getheri, na Mashi. Na Arfaksadi akamzaa Sala, na Sala akamzaa Eberi. Na Eberi akazaliwa wana wawili wa kiume; jina la wa kwanza aliitwa Pelegi, maana katika siku zake nchi iligawanyika; na jina la nduguye aliitwa Yoktani. Na Yoktani akamzaa Almodadi, na Shelefu, na Hasarmawethi, na Yera; na Hadoramu, na Uzali, na Dikla; na Obali, na Abimaeli, na Sheba; na Ofiri, na Havila, na Yobabu. Hao wote ndio wana wa Yoktani. Shemu, na Arfaksadi, na Sala; na Eberi, na Pelegi, na Reu; na Serugi, na Nahori, na Tera; na Abramu, naye ndiye Ibrahimu. Wana wa Ibrahimu; Isaka, na Ishmaeli. Hivi ndivyo vizazi vyao; mzaliwa wa kwanza wa Ishmaeli, Nebayothi; kisha Kedari, na Abdeeli, na Mibsamu; na Mishma, na Duma, na Masa, na Hadadi, na Tema; na Yeturi, na, Nafishi, na Kedema. Hao ndio wana wa Ishmaeli. Na wana wa Ketura, suria yake Ibrahimu; yeye akamzaa Zimrani, na Yokshani, na Medani, na Midiani, na Ishbaki, na Shua. Na wana wa Yokshani; Sheba na Dedani.
1 Mambo ya Nyakati 1:12-32 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Wapathrusi, Wakasluhi (hao ndio asili ya Wafilisti) na Wakaftori. Wana wa Kanaani walikuwa: Sidoni, mzaliwa wake wa kwanza, na Hethi, Wayebusi, Waamori, Wagirgashi, Wahivi, Waariki, Wasini, Waarvadi, Wasemari na Wahamathi. Wana wa Shemu walikuwa: Elamu, Ashuru, Arfaksadi, Ludi na Aramu. Wana wa Aramu walikuwa: Usi, Huli, Getheri na Mesheki. Arfaksadi akamzaa Shela, Shela akamzaa Eberi. Eberi alipata wana wawili: Mmoja wao aliitwa Pelegi, kwa kuwa wakati wake dunia iligawanyika; nduguye aliitwa Yoktani. Wana wa Yoktani walikuwa: Almodadi, Shelefu, Hasarmawethi, Yera, Hadoramu, Uzali, Dikla, Obali, Abimaeli, Sheba, Ofiri, Havila na Yobabu. Wote hawa walikuwa wana wa Yoktani. Wana wa Shemu walikuwa Arfaksadi, Shela, Eberi, Pelegi, Reu, Serugi, Nahori, Tera, Tera akamzaa Abramu (yaani, Abrahamu). Abrahamu alikuwa na wana wawili: Isaki na Ishmaeli. Hawa ndio waliokuwa wazao wa Hagari: Nebayothi mzaliwa wa kwanza wa Ishmaeli, Kedari, Adbeeli, Mibsamu, Mishma, Duma, Masa, Hadadi, Tema, Yeturi, Nafishi na Kedema. Hao ndio wana wa Ishmaeli. Wana waliozaliwa na Ketura suria wa Abrahamu walikuwa: Zimrani, Yokshani, Medani, Midiani, Ishbaki na Shua. Wana wa Yokshani walikuwa: Sheba na Dedani.