1
Luka MT. 3:21-22
New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921
Na watu wote walipokwisha kubatizwa, na Yesu nae akiisha kubatizwa, na akisali, mbingu zilifunuka. Roho Mtakatifu akashuka juu yake kwa mfano wa kiwiliwili kama hua, sauti ikatoka mbinguni, Wewe ndiwe mwana wangu, mpendwa wangu, ndiwe unipendezae.
Linganisha
Chunguza Luka MT. 3:21-22
2
Luka MT. 3:16
Yohana akajibu, akawaambia wote, Mimi nawabatiza kwa maji, lakini yuaja aliye hodari kuliko mimi, ambae kwamba mimi sistahili kumfungulia ukanda wa viatu vyake; yeye atawabatizeni kwa Roho Mtakatifu na kwa moto
Chunguza Luka MT. 3:16
3
Luka MT. 3:8
Zaeni, bassi, matunda yapatanayo na toba wala msianze kusema ndani ya nafsi zenu, Tunae baba ndiye Ibrahimu; kwa maana nawaambieni, ya kwamba Mungu katika mawe haya aweza kumwinulia Ibrahimu watoto.
Chunguza Luka MT. 3:8
4
Luka MT. 3:9
Na sasa hivi shoka limekwisha kutiwa katika shina la miti, bassi killa mti usiozaa matunda mema hukatwa ukatupwa motoni.
Chunguza Luka MT. 3:9
5
Luka MT. 3:4-6
kaina ilivyoandikwa katika chuo cha maneno ya nabii Isaya, Sauti yake apigae mbiu jangwani, Itengenezeni njia ya Bwana, Nyosheni mapito yake. Killa bonde litajazwa, Na killa jabali na mlima utashushwra, Palipopotoka patakuwa pamenyoka, Na njia zilizoparuza zitakuwa njia sawa; Na wote wenye mwili watanona wokofu wa Mungu.
Chunguza Luka MT. 3:4-6
Nyumbani
Biblia
Mipango
Video