Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Luka MT. 3

3
1HATTA katika mwaka wa kumi na tano wa kutawala kwake Tiberio Kaisari, Pontio Pilato alipokuwa liwali wa Yahudi, na Herode tetrarka wa Galilaya, na Filipo ndugu yake tetrarka wa Iturea, na wa inchi ya Trakoniti, na Lusania tetrarka wa Abilene, 2wakati wa ukuhani ukuu wa Anna na Kayafa, neno la Mungu likamfikia Yohana, mwana wa Zakaria, jangwani. 3Akalika inchi yote iliyo kando ya Yardani, akikhuhiri ubatizo wa toba liletalo ondoleo la dhambi, 4kaina ilivyoandikwa katika chuo cha maneno ya nabii Isaya,
Sauti yake apigae mbiu jangwani,
Itengenezeni njia ya Bwana,
Nyosheni mapito yake.
5Killa bonde litajazwa,
Na killa jabali na mlima utashushwra,
Palipopotoka patakuwa pamenyoka,
Na njia zilizoparuza zitakuwa njia sawa;
6Na wote wenye mwili watanona wokofu wa Mungu.
7Bassi akawaambia makutano waliotokea illi kubatizwa nae, Enyi uzao wa nyoka, ni nani aliyewaonya kuikimbia ghadhabu itakayokuja? 8Zaeni, bassi, matunda yapatanayo na toba wala msianze kusema ndani ya nafsi zenu, Tunae baba ndiye Ibrahimu; kwa maana nawaambieni, ya kwamba Mungu katika mawe haya aweza kumwinulia Ibrahimu watoto. 9Na sasa hivi shoka limekwisha kutiwa katika shina la miti, bassi killa mti usiozaa matunda mema hukatwa ukatupwa motoni. 10Nao makutano wakamwuliza wakinena, Tufanyeni, bassi? 11Akajibu akawaambia, Mwenye kanzu mbili na ampe yeye asiye nayo, na mwenye vyakula, na afanye vivyo hivyo. 12Watoza ushuru nao wakaja illi kubatizwa, wakamwambia, Mwalimu, tufanyeni? 13Akawaambia, Msifoze kitu zaidi ya vile mlivyoamriwa. 14Askari nao wakamwuliza wakisema, Nasi tufanyeni? Akawaambia, Msimtende jeuri mtu aliye yote, wala msitoze kitu bila haki; tena mwe radhi na mshsahara wenu.
15Bassi wale watu walipokuwa katika hali ya kutazamia, wakitafakari wote khabari za Yohana, kwamba yeye huenda akawa Kristo, 16Yohana akajibu, akawaambia wote, Mimi nawabatiza kwa maji, lakini yuaja aliye hodari kuliko mimi, ambae kwamba mimi sistahili kumfungulia ukanda wa viatu vyake; yeye atawabatizeni kwa Roho Mtakatifu na kwa moto: 17pepeto lake li mkononi mwake, nae ataitakasa sana sakafu yake; afakusanya nganu yake ghalani mwake, bali makapi atayateketeza kwa moto usiozimika.
18Bassi kwa maonyo mengi na ya namna nyingine mengi akawakhubiri watu. 19Lakini Herode tetrarka, akikaripiwa nae kwa ajili ya Herodias, mke wa Filipo, ndugu yake, na kwa ajili ya maovu yote aliyoyafanya Herode, 20akaongeza na hili jun ya yote, alimfunga Yohana gerezani. 21Na watu wote walipokwisha kubatizwa, na Yesu nae akiisha kubatizwa, na akisali, mbingu zilifunuka. 22Roho Mtakatifu akashuka juu yake kwa mfano wa kiwiliwili kama hua, sauti ikatoka mbinguni, Wewe ndiwe mwana wangu, mpendwa wangu, ndiwe unipendezae.
23Nae Yesu mwenyewe alipokuwa akianza kufundisha, umri wake amekuwa miaka thelathini, akidhaniwa kuwa mwana wa Yusuf, wa Eli, 24wa Mathati, wa Lawi, wa Melki, wa Yanna, wa Yusuf, 25wa Matathia, wa Amos, wa Nahum, wa Esli, wa Nagai, 26wa Maathi, wa Matathia, wa Semei, wa Yosef, wa Yuda, 27wa Yohana, wa Resa, wa Zorobabel, wa Salathiel, wa Neri, 28wa Melki, wa Addi, wa Kosan, wa Elmadam, wa Eri, 29wa Yesua, wa Eliezer, wa Yorim, wa Mathati, wa Lawi, 30wa Sumeon, wa Yuda, wa Yusuf, wa Yona, wa Eliakim, 31wa Melea, wa Mainan, wa Mattatha, wa Nathan, wa Daud, 32wa Yese, wa Obed, wa Boaz, wa Salmon, wa Nahason, 33wa Aminadab, wa Aram, wa Esrom, wa Fares, wa Yuda, 34wa Yakob, wa Isaak, wa Ibrahimu, wa Tara, wa Nahor, 35wa Saruhu, wa Ragau, wa Faleg, wa Eber, wa Sala, 36wa Kainan, va Arfaksad, wa Sem, wa Nuhu, wa Lamek, 37wa Methusala, wa Enok, wa Yared, wa Maleleel, wa Kainan, 38wa Enos, wa Seth, wa Adamu, wa Mungu.

Iliyochaguliwa sasa

Luka MT. 3: SWZZB1921

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia