Akamwongoza hatta Yerusalemi, akamweka juu ya ukumbi wa hekalu, akamwambia, Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu, jitupe chini, toka huku: maana imeandikwa,
Atakuagizia malaika zake wakulinde,
na, Mikononi mwao watakuchukua,
Usije ukajikwaa mguu wako kalika jiwe.
Yesu akajibu akamwambia, Imenenwa, Usimjaribu Bwana Mungu wako.