1
Yak 3:17
Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia
Lakini hekima itokayo juu, kwanza ni safi, tena ni ya amani, ya upole, tayari kusikiliza maneno ya watu, imejaa rehema na matunda mema, haina fitina, haina unafiki.
Linganisha
Chunguza Yak 3:17
2
Yak 3:13
N’nani aliye na hekima na ufahamu kwenu? Na aonyeshe kazi zake kwa mwenendo wake mzuri, katika upole wa hekima.
Chunguza Yak 3:13
3
Yak 3:18
Na tunda la haki hupandwa katika amani na wale wafanyao amani.
Chunguza Yak 3:18
4
Yak 3:16
Maana hapo palipo wivu na ugomvi ndipo palipo machafuko, na kila tendo baya.
Chunguza Yak 3:16
5
Yak 3:9-10
Kwa huo twamhimidi Mungu Baba yetu, na kwa huo twawalaani wanadamu waliofanywa kwa mfano wa Mungu. Katika kinywa kile kile hutoka baraka na laana. Ndugu zangu, haifai mambo hayo kuwa hivyo.
Chunguza Yak 3:9-10
6
Yak 3:6
Nao ulimi ni moto; ule ulimwengu wa uovu, ule ulimi, umewekwa katika viungo vyetu, nao ndio uutiao mwili wote unajisi, huuwasha moto mfulizo wa maumbile, nao huwashwa moto na jehanum.
Chunguza Yak 3:6
7
Yak 3:8
Bali ulimi hakuna awezaye kuufuga; ni uovu usiotulia, umejaa sumu iletayo mauti.
Chunguza Yak 3:8
8
Yak 3:1
Ndugu zangu, msiwe waalimu wengi, mkijua ya kuwa mtapata hukumu kubwa zaidi.
Chunguza Yak 3:1
Nyumbani
Biblia
Mipango
Video