Mwanangu, kama utayakubali maneno yangu
na kuyaweka akiba maagizo yangu ndani mwako,
kutega sikio lako kwenye hekima
na kuweka moyo wako katika ufahamu,
na kama utaiita busara,
na kuita kwa sauti upate ufahamu,
na ukiitafuta kama fedha
na kuitafuta sana kama hazina iliyofichwa,
ndipo utakapoelewa kumcha Mwenyezi Mungu
na kupata maarifa ya Mungu.