1
Mithali 3:5-6
Neno: Maandiko Matakatifu 2024
Mtumaini Mwenyezi Mungu kwa moyo wako wote wala usizitegemee akili zako mwenyewe; katika njia zako zote mkiri yeye, naye atayanyoosha mapito yako.
Linganisha
Chunguza Mithali 3:5-6
2
Mithali 3:7
Usiwe mwenye hekima machoni pako mwenyewe; mche Mwenyezi Mungu ukajiepushe na uovu.
Chunguza Mithali 3:7
3
Mithali 3:9-10
Mheshimu Mwenyezi Mungu kwa mali yako na kwa malimbuko ya mazao yako yote; ndipo ghala zako zitakapojaa hadi kufurika, viriba vyako vitafurika kwa mvinyo mpya.
Chunguza Mithali 3:9-10
4
Mithali 3:3
Usiache kamwe upendo na uaminifu vitengane nawe; vifunge shingoni mwako, viandike katika ubao wa moyo wako.
Chunguza Mithali 3:3
5
Mithali 3:11-12
Mwanangu, usidharau adhabu ya Mwenyezi Mungu na usichukie maonyo yake, kwa sababu Mwenyezi Mungu huwaadibisha wale anaowapenda, kama vile baba afanyavyo kwa mwana apendezwaye naye.
Chunguza Mithali 3:11-12
6
Mithali 3:1-2
Mwanangu, usisahau mafundisho yangu, bali zitunze amri zangu moyoni mwako, kwa kuwa zitakuongezea miaka mingi ya maisha yako na kukuletea mafanikio.
Chunguza Mithali 3:1-2
7
Mithali 3:13-15
Heri mtu yule apataye hekima, mtu yule apataye ufahamu, kwa maana hekima ana faida kuliko fedha na mapato yake ni bora kuliko ya dhahabu safi. Hekima ana thamani kuliko marijani; hakuna chochote unachokitamani kinachoweza kulinganishwa naye.
Chunguza Mithali 3:13-15
8
Mithali 3:27
Usizuie wema kwa wale wanaostahili ikiwa katika uwezo wako kutenda.
Chunguza Mithali 3:27
9
Mithali 3:19
Kwa hekima Mwenyezi Mungu aliiweka misingi ya dunia, kwa ufahamu aliziweka mbingu mahali pake
Chunguza Mithali 3:19
Nyumbani
Bibilia
Mipango
Video