1
Walawi 26:12
Neno: Bibilia Takatifu 2025
NENO
Nitatembea kati yenu niwe Mungu wenu, nanyi mtakuwa watu wangu.
Linganisha
Chunguza Walawi 26:12
2
Walawi 26:4
nitawanyeshea mvua katika majira yake, nayo ardhi itatoa mazao yake, na miti ya mashambani itazaa matunda yake.
Chunguza Walawi 26:4
3
Walawi 26:3
“ ‘Ikiwa mtafuata amri zangu na kuwa waangalifu kutii maagizo yangu
Chunguza Walawi 26:3
4
Walawi 26:6
“ ‘Nitawapa amani katika nchi, mpate kulala pasipo kutiwa hofu na yeyote. Nitawaondoa wanyama wakali watoke kwenye nchi, nao upanga hautapita katika nchi yenu.
Chunguza Walawi 26:6
5
Walawi 26:9
“ ‘Nitawaangalia kwa upendeleo na kuwafanya mzae na kuzidisha idadi yenu, nami nitalishika agano langu na ninyi.
Chunguza Walawi 26:9
6
Walawi 26:13
Mimi ndimi BWANA Mungu wenu, niliyewatoa katika nchi ya Misri ili msiendelee kuwa watumwa wa Wamisri, nikavunja nira yenu, na kuwawezesha kutembea mkiwa mmeinua vichwa vyenu.
Chunguza Walawi 26:13
7
Walawi 26:11
Nitafanya makao yangu miongoni mwenu, nami sitawachukia.
Chunguza Walawi 26:11
8
Walawi 26:1
“ ‘Msijitengenezee sanamu, au kusimamisha sanamu ya kuchonga, au jiwe la kuabudia, na pia msijiwekee jiwe lililochongwa katika nchi yenu ili kulisujudia. Mimi ndimi BWANA Mungu wenu.
Chunguza Walawi 26:1
9
Walawi 26:10
Wakati wa kuvuna mtakuwa bado mnakula mavuno ya mwaka uliopita, na itawalazimu kuyaondoa ghalani ili mpate nafasi ya mavuno mapya.
Chunguza Walawi 26:10
10
Walawi 26:8
Watu wenu watano watafukuza adui mia moja, na watu wenu mia moja watafukuza adui elfu kumi, nao adui zenu wataanguka kwa upanga mbele yenu.
Chunguza Walawi 26:8
11
Walawi 26:5
Kupura nafaka kwenu kutaendelea hadi wakati wa kuvuna zabibu. Na kuvuna zabibu kutaendelea hadi wakati wa kupanda mbegu, nanyi mtakula na kushiba, na mtaishi salama katika nchi yenu.
Chunguza Walawi 26:5
12
Walawi 26:7
Mtawafukuza adui zenu, nanyi mtawaua kwa upanga mbele yenu.
Chunguza Walawi 26:7
13
Walawi 26:2
“ ‘Zishikeni Sabato zangu na kuheshimu mahali patakatifu pangu. Mimi ndimi BWANA.
Chunguza Walawi 26:2
Nyumbani
Biblia
Mipango
Video