Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu:
“Mwenye hekima asijisifu katika hekima yake,
au mwenye nguvu ajisifu katika nguvu zake,
wala tajiri ajisifu katika utajiri wake,
lakini yeye ajisifuye, na ajisifu kwa sababu hii:
kwamba ananifahamu na kunijua mimi,
kwamba mimi ndimi Mwenyezi Mungu, nitendaye wema,
hukumu na haki duniani,
kwa kuwa napendezwa na haya,”
asema Mwenyezi Mungu.