1
Isaya 9:6
Neno: Maandiko Matakatifu 2024
Kwa maana, kwa ajili yetu mtoto amezaliwa, tumepewa mtoto wa kiume, nao utawala utakuwa begani mwake. Naye ataitwa Mshauri wa Ajabu, Mungu Mwenye Nguvu, Baba wa Milele, Mfalme wa Amani.
Linganisha
Chunguza Isaya 9:6
2
Isaya 9:2
Watu wanaotembea katika giza wameona nuru kuu, wale wanaoishi katika nchi ya uvuli wa mauti, nuru imewazukia.
Chunguza Isaya 9:2
3
Isaya 9:7
Kuongezeka kwa utawala wake na amani hakutakuwa na mwisho. Atatawala kwenye kiti cha utawala cha Daudi na juu ya ufalme wake, akiuthibitisha na kuutegemeza kwa haki na kwa adili, tangu wakati huo na hata milele. Wivu wa Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni utatimiza haya.
Chunguza Isaya 9:7
4
Isaya 9:5
Kila kiatu cha shujaa kilichotumiwa vitani, na kila vazi lililovingirishwa katika damu vitawekwa kwa ajili ya kuchomwa, vitakuwa kuni za kuwasha moto.
Chunguza Isaya 9:5
5
Isaya 9:1
Hata hivyo, hakutakuwa huzuni tena kwa wale waliokuwa katika dhiki. Hapo awali aliidhili nchi ya Zabuloni na nchi ya Naftali, lakini katika siku zijazo ataipa heshima Galilaya ya Mataifa, karibu na njia ya bahari, ng’ambo ya Yordani
Chunguza Isaya 9:1
6
Isaya 9:3
Umelikuza taifa, na kuzidisha furaha yao, wanafurahia mbele zako, kama watu wanavyofurahia wakati wa mavuno, kama mashujaa wanavyofurahia wakigawanya nyara.
Chunguza Isaya 9:3
7
Isaya 9:4
Kama vile siku ya kushindwa kwa Wamidiani, umevunja nira iliyowalemea, ile gongo mabegani mwao na fimbo ya aliyewadhulumu.
Chunguza Isaya 9:4
Nyumbani
Bibilia
Mipango
Video