Walipofika Mara, hawakuweza kunywa maji yake kwa sababu yalikuwa machungu. (Ndiyo sababu mahali hapo panaitwa Mara) Kwa hiyo watu wakamnungʼunikia Mose, wakisema, “Tunywe nini?”
Ndipo Mose akamlilia BWANA, naye BWANA akamwonyesha kipande cha mti. Akakitupa ndani ya maji, nayo maji yakawa matamu.
Huko BWANA akawapa amri na sheria na huko akawajaribu.