Kutoka 15:23-25
Kutoka 15:23-25 Biblia Habari Njema (BHN)
Walipofika mahali panapoitwa Mara, hawakuweza kuyanywa maji ya Mara kwa sababu yalikuwa machungu. Kwa sababu hiyo mahali hapo pakaitwa Mara. Basi, watu wote wakamlalamikia Mose wakisema, “Sasa tutakunywa nini?” Hapo Mose akamlilia Mwenyezi-Mungu, naye akamwonesha kipande cha mti, na Mose akakitumbukiza katika maji; maji hayo yakawa mazuri. Huko Mungu aliwapa Waisraeli amri na agizo, ili ajue uthabiti wao
Kutoka 15:23-25 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Walipofika mahali palipoitwa Mara hawakupata kuyanywa yale maji ya Mara, kwa kuwa yalikuwa machungu; kwa ajili ya hayo jina lake likaitwa Mara Ndipo watu wakamnung'unikia Musa, wakisema, Tunywe nini? Naye akamlilia BWANA; BWANA akamwonesha mti, naye akautia katika hayo maji, maji yakawa matamu. Basi akawawekea amri na hukumu huko, akawajaribu huko
Kutoka 15:23-25 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Walipofika mahali palipoitwa Mara hawakupata kuyanywa yale maji ya Mara, kwa kuwa yalikuwa machungu; kwa ajili ya hayo jina lake likaitwa Mara. Ndipo watu wakamnung’unikia Musa, wakisema, Tunywe nini? Naye akamlilia BWANA; BWANA akamwonyesha mti, naye akautia katika hayo maji, maji yakawa matamu. Basi akawawekea amri na hukumu huko, akawaonja huko
Kutoka 15:23-25 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Walipofika Mara, hawakuweza kunywa maji yake kwa sababu yalikuwa machungu. (Ndiyo sababu mahali hapo panaitwa Mara) Kwa hiyo watu wakamnungʼunikia Mose, wakisema, “Tunywe nini?” Ndipo Mose akamlilia BWANA, naye BWANA akamwonyesha kipande cha mti. Akakitupa ndani ya maji, nayo maji yakawa matamu. Huko BWANA akawapa amri na sheria na huko akawajaribu.