Kwa siku sita utafanya kazi na kutenda shughuli zako zote. Lakini siku ya saba ni Sabato kwa Mwenyezi Mungu, Mungu wako. Siku hiyo hutafanya kazi yoyote, wewe, wala mwanao au binti yako, wala mtumishi wa kiume au wa kike, wala ng’ombe wako, punda wako au mnyama wako yeyote, wala mgeni aliye malangoni mwako, ili mtumishi wako wa kiume na wa kike wapate kupumzika kama wewe.