Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Mt 6:5
Hatua Zako za Mwanzo
Siku 5
Umefanya uamuzi wa kumfuata Yesu, sasa nini kinafuata? Mpango huu si orodha kamili ya kila kitu kinachokuja kutokana na uamuzi huo, lakini utakusaidia kuchukua hatua zako za kwanza.
Kutafuta Karoti
Siku 7
Wote tunatafuta kitu. Mara nyingi ni kitu ambacho hakipatikani--kazi nzuri, nyumba bora zaidi, familia bora, kukubalika na wengine. Lakini hii haichoshi? Je, kuna njia bora zaidi? Pata katika mpango wa new Life.Church Bible, ikifuatana na mfululizo wa ujumbe wa Mchungaji Craig Groeschel’s, Kutafuta Karoti.
Maombi Hatari
Siku 7
Umechoka kujali usalama katika imani yako? Uko tayari kukabili hofu zako, kujenga imani yako, na kufikia uwezo wako kamili? Mpango huu wa Biblia wa siku 7 kutoka kwenye kitabu cha Mchungaji Craig Groeschel wa Life.Church, "Dangerous Prayers" yaani Maombi Hatari, unakujasiri uombe bila kujali usalama—kwa sababu kumfuata Yesu haukufaa kuwa salama salmini.
Mafunzo ya Yesu
Siku 7
Yesu alifunza kuhusu mada nyingi- baraka zinazodumu, uzinzi, maombi na mengi zaidi. Ina maana gani kwa watu wa leo? Video fupi yaeleza kila upande wa hadithi kwa kila siku ya mpango huu.
Siku 21 za Kufunga
Siku 21
Anza mwaka mpya kwa kulenga nidhamu ya kiroho ya kufunga. Mpango huu unajumuisha vifungu kadhaa kuhusu kufunga, vingine vinahimiza kutafakari ukaribu na Mungu. Kwa siku 21, utapata somo la Biblia la kila siku, ibada fupi, maswali ya kutafakari, na maombi.
Maombi
Siku 21
Kujifunza namns ya kuomba vizuri, kutoka kwa maombi ya mwaminifi pia na maneno ya Yesu Mwenyewe. Kupata faraja ya kuendelea kuomba Mungu kila siku, pamoja na kudumu na uvumilivu. Chunguza mifano tupu, maombi ya uhaki wa mwenyewe, ikipimwa na maombi ya kweli ya walio na moyo safi. Omba bila kuacha.
Mpango Bora wa Kusoma
Siku 28
unajisihisi umezidiwa, kutoridhika, na kukwama maishani? Je unatamani maisha yako ya kila siku yaboreke? Neno la Mungu ni mwongozo kwa siku njema. Katika mpango huu wa siku 28, utagundua njia kutoka kuishi tu maisha mema, hadi kuishi maisha mema ambayo Mungu amekutazamia.
SOMA BIBLIA KILA SIKU 01/20
Siku 31
Soma Biblia Kila Siku 01/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Mathayo, Kutoka, Zaburi na Isaya. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Anza mwaka wa 2020 kwa kujifunza Neno la Mungu kupitia mpango huu.