YouVersion Logo
Search Icon

Soma Biblia Kila Siku/AGOSTI 2023Sample

Soma Biblia Kila Siku/AGOSTI 2023

DAY 20 OF 31

Kutokuamini kwa Mafarisayo kulisababisha Bwana Yesu awaambie kwa kutumia mfano wa mwizi na mchungaji wa kondoo waingiavyo na kuwafanyia kondoo. Mwizi anapowaendea kondoo hapitii mlangoni bali huparamia popote, na lengo lake niaibe na kuchinja na kuharibu(m.10). Mchungaji wa kondoo hupitia mlangoni. Anawafahamu kondoo kwa majina na kondoo wanaifahamu sauti yake, na lengo lake ni kuwaongoza kwenye malisho tele.Naye awatoapo nje kondoo wake wote, huwatangulia; na wale kondoo humfuata, kwa maana waijua sauti yake. ... Mimi ndimi mlango; mtu akiingia kwa mimi, ataokoka; ataingia na kutoka, naye atapata malisho(m.4 na 9). Je, nawe waisikia sauti ya mchungaji wa kondoo na kumfuata?

Scripture

Day 19Day 21

About this Plan

Soma Biblia Kila Siku/AGOSTI 2023

Soma Biblia Kila Siku Agosti 2023 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kuelewa somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu Yohana na Mithali. Karibu kujiunga na mpango huu.

More