YouVersion Logo
Search Icon

Siku Saba Za Kufanya Sala Wakati Upitiapo MajonziSample

Siku Saba Za Kufanya Sala Wakati Upitiapo Majonzi

DAY 5 OF 7

Twaa Ngao Ya Imani.

Tuombe,

Bwana, kwa mikono iliyochoka kwa huzuni, ninainua ngao ya imani ninaposhinda huzuni ninayohisi. Na Shetani, kwa jina la Kristo, ninakataa kuruhusu huzuni hii igeuke na kuwa uchungu. Ninajua mbinu zako, na haziwezi kufanya kazi kwangu mimi. Kwa ngao ya imani, ninakataa kila uwongo kuhusu hasara yangu na kupona kwangu. Nimepata hasara hapo awali, na nikapona. Nimepata fursa nyingine mpya za kicheko na matumaini wakati sikufikiri kuwa ningeweza kuwa nayo. Nitapitia haya kwa sababu Kristo ndani yangu ndiye tumaini la utukufu. Katika jina la Kristo, amina.

Scripture

Day 4Day 6

About this Plan

Siku Saba Za Kufanya Sala Wakati Upitiapo Majonzi

Siku 7 za Sala zimeundwa kwa minajili ya kuimarisha roho yako na kuhimiza moyo wako wakati upitiapo majonzi. Kila siku inajumuisha sala utakayofanya wewe au kutumia kama msingi wa maombi yako kuhusu mada ya siku hiyo ili kupata nafuu kutokana na majonzi. Katika siku hizi 7 utapata tumaini kutoka kwenye Neno la Mungu na kutiwa moyo kwa kujua kwamba upendo wake na faraja ni zako katika hali yoyote.

More