YouVersion Logo
Search Icon

Soma Biblia Kila Siku Julai 2021Sample

Soma Biblia Kila Siku Julai 2021

DAY 30 OF 31

Kila mmoja wetu ameonja namna fulani ya ugumu katika maisha. Kama wewe ni mmojawapo je, unafanyaje ili kushinda hali hii? Mfalme Daudi alitambua kwamba Mungu ndiye kimbilio lake, kwani hakuna wa kufanana naye. Nasi tupatwapo na matatizo tujiangalie tusije tukategemea njia za uovu wala miungu mingine. Tukumbuke ilivyoandikwa katika m.4: Heri aliyemfanya Bwana kuwa tumaini lake, wala hakuwaelekea wenye kiburi, wala hao wanaogeukia uongo. Tumwambie Mungu, tumngoje kwa saburi naye atasikia kilio chetu, atatupandisha toka shimo la uharibifu na kuisimamisha miguu yetu mwambani, kama mtunzi zaburi anavyoshuhudia katika m.1-2: Nalimngoja Bwana kwa saburi, akaniinamia akakisikia kilio changu. Akanipandisha toka shimo la uharibifu, toka udongo wa utelezi; akaisimamisha miguu yangu mwambani, akaziimarisha hatua zangu.

Scripture

Day 29Day 31

About this Plan

Soma Biblia Kila Siku Julai 2021

Soma Biblia Kila Siku Julai 2021 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Marko na Ezekieli. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu

More