YouVersion Logo
Search Icon

Soma Biblia Kila Siku Julai 2021Sample

Soma Biblia Kila Siku Julai 2021

DAY 26 OF 31

Chanzo cha dhiki ya Mwimba Zaburi kiko nje yake, lakini mateso yake yanayofungamana na dhiki hiyo anayasikia kwa namna mbili: 1. Kutoka nje anaona watesi na hata marafiki wasaliti (m.11, Kwa sababu ya watesi wangu nimekuwa laumu, naam, hasa kwa jirani zangu; na kitu cha kutisha kwa rafiki zangu; walioniona njiani walinikimbia). 2. Kutoka ndani yake, Mwimba Zaburi anaona maisha yake yanakatishwa na nguvu zake kutetemeka kwa sababu ya uovu uliompata. Dhiki yake ikiwa kuu hivi, Mwimba Zaburi anafuata kawaida yake: Anazidi kumtumainia Bwana (m.14-15, Mimi nakutumaini Wewe, Bwana, nimesema, Wewe ndiwe Mungu wangu. Nyakati zangu zimo mikononi mwako; uniponye na adui zangu, nao wanaonifuatia). Je, una dhiki? Tegemea wokovu wa Bwana kwa ajili ya fadhili zake. Angalia ombi katika m.16 ambalo unaweza kuliomba wewe pia: Umwangaze mtumishi wako kwa nuru ya uso wako; uniokoe kwa ajili ya fadhili zako.

Day 25Day 27

About this Plan

Soma Biblia Kila Siku Julai 2021

Soma Biblia Kila Siku Julai 2021 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Marko na Ezekieli. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu

More