YouVersion Logo
Search Icon

Soma Biblia Kila Siku Julai 2021Sample

Soma Biblia Kila Siku Julai 2021

DAY 28 OF 31

Tukio la 1 Sam 21:10-22:2 linatupa sababu ya Daudi kutunga zaburi hii. Zaidi ya sifa na shukrani (m.1-10) anatoa mafundisho kwa watu wa Mungu (m.11-22). Onjeni mwone ya kuwa Bwana yu mwema (m.8). Je, msomaji, umeonja? Ukiona embe, huwezi kujua kama ni jema bila kwanza kula kidogo, yaani, kuonja. Daudi alikuwa ametegemea Bwana siku za furaha na ziku za taabu na hofu. Alikuwa ameonja! Akatunga zaburi hii ili tumsifu Bwana pamoja naye. Maana alimwokoa wakati alipomlilia  katika taabu yake!

Day 27Day 29

About this Plan

Soma Biblia Kila Siku Julai 2021

Soma Biblia Kila Siku Julai 2021 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Marko na Ezekieli. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu

More