YouVersion Logo
Search Icon

Zaburi 141

141
Sala ya kutaka kulindwa kutoka kwenye uovu
1Ee BWANA, nimekuita, unijie hima,
Uisikie sauti yangu nikuitapo.
2 # Efe 5:2; 1 Tim 2:8; Ufu 5:8 Sala yangu ipae mbele zako kama uvumba,
Kuinuliwa mikono yangu kama dhabihu ya jioni.
3Ee BWANA, uweke mlinzi kinywani pangu,
Mngojezi mlangoni pa midomo yangu.
4 # Mt 6:14; 20:15; Mit 23:6 Usiuelekeze moyo wangu kunako jambo baya,
Nisiyazoelee matendo yasiyofaa,
Pamoja na watu watendao maovu;
Wala nisile vyakula vyao vya anasa.
5Mwenye haki na anipige, itakuwa fadhili;
Anikemee, itakuwa kama mafuta kichwani;
Kichwa changu kisikatae,
Maana siachi kusali kati ya mabaya yao.
6Wakuu wao wakiangushwa kando ya genge,
Watayasikia maneno yangu, maana ni matamu.
7 # 2 Kor 1:9 Kama kupasua kuni na kuzichanja juu ya nchi,
Ndivyo ilivyo mifupa yetu mdomoni pa kuzimu.
8 # Zab 25:15 Macho yangu yanakuelekea Wewe, MUNGU Bwana,
Nimekukimbilia Wewe, usiniache bila kinga.
9Unilinde kutoka kwa mtego walionitegea,
Na kutoka kwa matanzi ya watendao maovu.
10 # Est 7:10; Zab 7:15 Wabaya na waanguke katika nyavu zao wenyewe,
Wakati ninapopita salama.

Currently Selected:

Zaburi 141: SRUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in