YouVersion Logo
Search Icon

Zaburi 140

140
Sala ya ukombozi kutoka kwa adui
Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi.
1Ee BWANA, uniokoe kutoka kwa watu waovu.
Unihifadhi kutoka kwa watu wajeuri.
2Waliowaza mabaya mioyoni mwao,
Kila siku huchochea vita.
3 # Rum 3:13 Wamenoa ndimi zao na kuwa kama za nyoka,
Na katika midomo yao mna sumu ya fira.
4Ee BWANA, unilinde Kutoka kwa mikono ya mtu asiye haki;
Unihifadhi na watu wajeuri;
Waliopanga kuniangusha.
5 # Zab 10:9; Yer 18:22; Lk 11:53-54 Wenye kiburi wamenifichia mtego na kamba;
Wametandika wavu kando ya njia;
Wameniwekea matanzi.
6 # Zab 16:2 Nimemwambia BWANA, Ndiwe Mungu wangu;
Ee BWANA, uisikie sauti ya dua zangu.
7 # Kum 33:27-29; Zab 18:32 Ee MUNGU Bwana, nguvu za wokovu wangu,
Umenifunika kichwa changu siku ya vita.
8 # Ayu 5:12,13 Ee BWANA, usimpe asiye haki tamaa zake,
Usiifanikishe hila yake, wasije wakajiinua.
9 # Zab 7:16 Nao wainuapo vichwa watu wanaonizunguka,
Madhara ya midomo yao yawafunike.
10 # Zab 11:6 Makaa ya moto yawaangukie, watupwe motoni,
Na katika mashimo, wasipate kusimama tena.
11Msingiziaji hatawekwa imara katika nchi,
Mtu wa jeuri, uovu humwinda kumwangamiza.
12 # Zab 109:31 Najua ya kuwa BWANA atamfanyia mnyonge hukumu,
Na wahitaji haki yao.
13Hakika wenye haki watalishukuru jina lako,
Wenye adili watakaa mahali ulipo Wewe.

Currently Selected:

Zaburi 140: SRUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in