YouVersion Logo
Search Icon

Zab 57

57
Sifa na Hakikisho katika Mateso
Kwa mwimbishaji: kwa mtindo wa Usiharibu. Utenzi wa Daudi alipomponyoka Sauli na kujificha pangoni.
1 # Isa 26:20 Unirehemu, Ee Mungu, unirehemu mimi,
Maana nafsi yangu imekukimbilia Wewe.
Nitaukimbilia uvuli wa mbawa zako,
Hata misiba hii itakapopita.
2 # Zab 138:8 Nitamwita MUNGU Aliye juu,
Mungu anitimiziaye mambo yangu.
3 # Zab 144:5; 40:11 Atapeleka toka mbinguni na kuniokoa,
Atukanapo yule atakaye kunimeza.
Mungu atazipeleka
Fadhili zake na kweli yake
4 # Mit 30:14; Zab 64:3 Nafsi yangu i kati ya simba,
Nitastarehe kati yao waliowaka moto.
Wanadamu meno yao ni mikuki na mishale,
Na ndimi zao ni upanga mkali.
5 # Zab 108:5 Ee Mungu, utukuzwe juu ya mbingu,
Na juu ya nchi yote uwe utukufu wako.
6 # Zab 9:15 Wameweka wavu ili kuninasa miguu;
Nafsi yangu imeinama;
Wamechimba shimo mbele yangu;
Wametumbukia ndani yake!
7 # Zab 108:1 Ee Mungu, moyo wangu u thabiti,
Moyo wangu u thabiti.
Nitaimba, nitaimba zaburi,
8 # Amu 5:12 Amka, utukufu wangu.
Amka, kinanda na kinubi,
Nitaamka alfajiri.
9Ee Bwana, nitakushukuru kati ya watu,
Nitakuimbia zaburi kati ya mataifa.
10 # Zab 108:4 Maana fadhili zako ni kubwa hata mbinguni,
Na uaminifu wako hata mawinguni.
11Ee Mungu, utukuzwe juu ya mbingu,
Na juu ya nchi yote uwe utukufu wako.

Currently Selected:

Zab 57: SUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in