YouVersion Logo
Search Icon

Zab 56

56
Kumtumaini Mungu katika Mateso
Kwa mwimbishaji: kwa mtindo wa Njiwa Mkimya wa Mbali. Utenzi wa Daudi alipokamatwa na Wafilisti kule Gathi.
1 # Zab 31:9 Mungu, unirehemu, maana yuko atakaye kunimeza,
Mchana kutwa ananionea akileta vita.
2 # Zab 57:3 Adui zangu wanataka kunimeza mchana kutwa,
Maana waletao vita juu yangu kwa kiburi ni wengi.
3 # 1 Sam 30:6; 2 Nya 20:3 Siku ya hofu yangu nitakutumaini Wewe;
4 # Ebr 13:5,6 Kwa msaada wa MUNGU nitalisifu neno lake.
Nimemtumaini Mungu, sitaogopa;
Mwenye mwili atanitenda nini?
5Mchana kutwa wanapotosha maneno yangu,
Mawazo yao yote ni juu yangu kunitakia mabaya.
6 # Mdo 4:27,28 Hukutanika, hujificha, huziangalia nyayo zangu,
Kwa kuwa wameniotea nafsi yangu.
7Je! Wataokoka kwa uovu wao?
Ee Mungu, uwaangamize kwa hasira yako.
8 # Mal 3:16 Umehesabu kutanga-tanga kwangu;
Uyatie machozi yangu katika chupa yako;
(Je! Hayamo katika kitabu chako?)
9 # Isa 8:9,10 Ndipo adui zangu watarudi nyuma siku ile niitapo.
Neno hili najua kuwa MUNGU yu upande wangu;
10Kwa msaada wa MUNGU nitalisifu neno lake.
Kwa msaada wa BWANA nitalisifu neno lake.
11Nimemtumaini Mungu, sitaogopa;
Mwanadamu atanitenda nini?
12 # Zab 116:14-16 Ee Mungu, nadhiri zako zi juu yangu;
Nitakutolea dhabihu za kushukuru.
13 # Ayu 33:30 Maana umeniponya nafsi yangu na mauti;
Je! Hukuizuia miguu yangu isianguke?
Ili nienende mbele za Mungu
Katika nuru ya walio hai.

Currently Selected:

Zab 56: SUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in