Zab 58
58
Sala ya Kutaka Kisasi
Kwa mwimbishaji: kwa mtindo wa Usiharibu. Utenzi wa Daudi.
1Ni kweli, enyi wakuu, mnanena haki?
Enyi wanadamu, mnahukumu kwa adili?
2 #
Zab 94:20
Sivyo! Mioyoni mwenu mnatenda maovu;
Katika nchi mnapima udhalimu wa mikono yenu.
3 #
Zab 51:5
Wasio haki wamejitenga tangu kuzaliwa kwao;
Tangu tumboni wamepotea, wakisema uongo.
4 #
Zab 140:4
Sumu yao, mfano wake ni sumu ya nyoka;
Mfano wao ni fira kiziwi azibaye sikio lake.
5Asiyeisikiliza sauti ya waganga,
Ijapo wanafanya uganga kwa ustadi.
6 #
Ayu 4:10
Ee Mungu, uyavunje meno yao vinywani mwao;
Ee BWANA, uyavunje magego ya wana-simba.
7Na watoweke kama maji yapitayo kwa kasi;
Akiielekeza mishale yake, iwe imetiwa ubutu.
8Kama konokono ayeyukaye na kutoweka,
Kama mimba iliyoharibika, isiyoliona jua,
9 #
Mit 10:25
Kabla ya masufuria yenu kupata moto wa miiba,
Ataipeperusha kama chamchela,
Iliyo mibichi na iliyo moto.
10 #
Kum 32:42; Ayu 22:19; Zab 18:47; Mit 10:11; Ufu 18:20 Mwenye haki atafurahi akionapo kisasi;
Ataiosha miguu yake katika damu ya wasio haki.
11 #
Rum 2:6-11; Ayu 34:11; Mhu 5:8; Yer 32:19; Eze 7:27; Rum 14:12; Ufu 2:23 Na mwanadamu atasema,
Hakika iko thawabu yake mwenye haki.
Hakika yuko Mungu
Anayehukumu katika dunia.
Currently Selected:
Zab 58: SUV
Highlight
Share
Copy
Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in
Swahili Union Version (SUV): © Bible Society of Tanzania and Bible Society of Kenya, 1952, 1997. All rights reserved. lt/pgt ltpgtSwahili Union Version (SUV): Hakimiliki -1952, 1997: kwa: Chama cha Biblia cha Tanzania na Chama cha Biblia cha Kenya. Haki zote zimehifadhiwa.