YouVersion Logo
Search Icon

Zab 113

113
Mungu Msaidizi wa Mhitaji
1Haleluya.
Enyi watumishi wa BWANA, sifuni,
Lisifuni jina la BWANA.
2 # Dan 2:20 Jina la BWANA lihimidiwe
Tangu leo na hata milele.
3 # Isa 59:19; Hab 2:14; Mal 1:11; Ufu 11:15 Toka maawio ya jua hata machweo yake
Jina la BWANA husifiwa.
4BWANA ni mkuu juu ya mataifa yote,
Na utukufu wake ni juu ya mbingu.
5Ni nani aliye mfano wa BWANA,
Mungu wetu aketiye juu;
6 # Isa 57:15 Anyenyekeaye kutazama,
Mbinguni na duniani?
7 # 1 Sam 2:8; Isa 26:19; Dan 12:2 Humwinua mnyonge kutoka mavumbini,
Na kumpandisha maskini kutoka jaani.
8 # Ayu 36:7 Amketishe pamoja na wakuu,
Pamoja na wakuu wa watu wake.
9 # 1 Sam 2:5; Gal 4:27 Huweka nyumbani mwanamke aliye tasa,
Awe mama ya watoto mwenye furaha.

Currently Selected:

Zab 113: SUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy