YouVersion Logo
Search Icon

Zab 106

106
Ungamo la Dhambi za Israeli
1 # 1 Nya 16:34; 2 Nya 5:13; 7:3; Ezr 3:11; Zab 100:5; 107:1; 118:1; 136:1; Isa 63:7; Yer 33:11; Mt 19:17 Haleluya.
Mshukuruni BWANA kwa kuwa ni mwema,
Kwa maana fadhili zake ni za milele.
2 # Zab 40:5 Nani awezaye kuyanena matendo makuu ya BWANA,
Kuzihubiri sifa zake zote?
3 # Yer 22:15,16; Mt 22:37; Zab 15:2; Mdo 24:16; Gal 6:9 Heri washikao hukumu,
Na kutenda haki sikuzote.
4Ee BWANA, unikumbuke mimi,
Kwa kibali uliyo nayo kwa watu wako.
Unijilie kwa wokovu wako,
5Ili niuone wema wa wateule wako.
Nipate kuifurahia furaha ya taifa lako,
Na kujisifu pamoja na watu wako.
6 # Law 26:40; 1 Fal 8:47; Dan 9:5 Tumetenda dhambi pamoja na baba zetu,
Tumetenda maovu, tumefanya ubaya.
7 # Kut 14:10-12 Baba zetu katika Misri
Hawakufikiri matendo yako ya ajabu;
Hawakukumbuka wingi wa fadhili zako;
Wakaasi penye bahari, bahari ya Shamu.
8 # Yos 7:9; Zab 143:11; Yer 14:7,21 Lakini akawaokoa kwa ajili ya jina lake,
Ayadhihirishe matendo yake makuu.
9 # Kut 14:21-31; Nah 1:4; Isa 63:11 Akaikemea bahari ya Shamu ikakauka,
Akawaongoza vilindini kana kwamba ni uwanda.
10Akawaokoa na mkono wa mtu aliyewachukia,
Na kuwakomboa na mkono wa adui zao.
11Maji yakawafunika watesi wao,
Hakusalia hata mmoja wao.
12 # Kut 15:1-21 Ndipo walipoyaamini maneno yake,
Waliziimba sifa zake.
13Wakayasahau matendo yake kwa haraka,
Hawakulingojea shauri lake.
14 # Hes 11:4-34 Bali walitamani sana jangwani,
Wakamjaribu Mungu nyikani.
15 # Isa 10:16 Akawapa walichomtaka,
Akawakondesha roho zao.
16 # Hes 16:1-35 Wakamhusudu Musa matuoni,
Na Haruni, mtakatifu wa BWANA.
17Nchi ikapasuka ikammeza Dathani,
Ikaufunika mkutano wa Abiramu.
18Moto ukawaka katika mkutano wao,
Miali yake ikawateketeza wabaya.
19 # Kut 32:1-14 Walifanya ndama huko Horebu,
Wakaisujudia sanamu ya kuyeyuka.
20 # Yer 2:11; Rum 1:23 Wakaubadili utukufu wao
Kuwa mfano wa ng’ombe mla majani.
21Wakamsahau Mungu, mwokozi wao,
Aliyetenda makuu katika Misri.
22Matendo ya ajabu katika nchi ya Hamu,
Mambo ya kutisha penye bahari ya Shamu.
23 # Kut 32:10; Kum 9:19; Eze 20:13; 13:5 Akasema ya kuwa atawaangamiza
Kama Musa, mteule wake, asingalisimama,
Mbele zake kama mahali palipobomoka,
Ili aigeuze hasira yake asije akawaharibu.
24 # Hes 14:1-35 Wakaidharau nchi ile ya kupendeza,
Wala hawakuliamini neno lake.
25Bali wakanung’unika hemani mwao,
Wala hawakuisikiliza sauti ya BWANA.
26Ndipo alipowainulia mkono wake,
Ya kuwa atawaangamiza jangwani,
27 # Law 26:33 Na kuwatawanya wazao wao kati ya mataifa,
Na kuwatapanya katika nchi mbali.
28 # Hes 25:1-13; Kum 4:3; Hos 9:10; Ufu 2:14 Wakajiambatiza na Baal-Peori,
Wakazila dhabihu za wafu.
29Wakamkasirisha kwa matendo yao;
Tauni ikawashambulia.
30Ndipo Finehasi akasimama akafanya hukumu;
Tauni ikazuiliwa.
31Akahesabiwa kuwa ana haki
Kizazi baada ya kizazi hata milele.
32 # Hes 20:2-13; Yak 3:2 Wakamghadhibisha penye maji ya Meriba,
Hasara ikampata Musa kwa ajili yao,
33Kwa sababu waliiasi roho yake,
Akasema yasiyofaa kwa midomo yake.
34 # Amu 1:21; 2:1-3; 3:5-6; Kum 7:2 Hawakuwaharibu watu wa nchi
Kama BWANA alivyowaambia;
35 # Amu 3:5; Isa 2:6 Bali walijichanganya na mataifa,
Wakajifunza matendo yao.
36 # Kut 23:33; Kum 7:10; Amu 2:12; 2 Fal 17:8-11; 2 Nya 33:2-7 Wakazitumikia sanamu zao,
Nazo zikawa mtego kwao.
37 # Kum 12:30,31; Isa 57:5; Eze 16:20; 2 Fal 17:17 Naam, walitoa wana wao na binti zao
Kuwa dhabihu kwa mashetani.
38 # Hes 35:33 Wakamwaga damu isiyo na hatia,
Damu ya wana wao na binti zao,
Waliowatoa dhabihu kwa sanamu za Kanaani;
Nchi ikatiwa unajisi kwa damu.
39Ndivyo walivyotiwa uchafu kwa kazi zao,
Wakafanya uasherati kwa matendo yao.
40 # Amu 2:14-18 Hasira ya BWANA ikawaka juu ya watu wake,
Akauchukia urithi wake.
41 # Amu 2:14; Neh 9:27 Akawatia mikononi mwa mataifa,
Nao waliowachukia wakawatawala.
42Adui zao wakawaonea,
Wakatiishwa chini ya mkono wao.
43Mara nyingi aliwaponya,
Bali walikuwa wakimwasi kwa mashauri yao,
Wakadhilika katika uovu wao.
44 # Amu 10:10 # Law 26:41; Omb 3:32 Lakini aliyaangalia mateso yao,
Aliposikia kilio chao.
45Akawakumbukia agano lake;
Akawahurumia kwa wingi wa fadhili zake;
46 # Ezr 9:9; Yer 42:12 Akawajalia kuhurumiwa
Na watu wote waliowateka.
47 # 1 Nya 16:35-36; 2 Nya 5:13; Lk 1:74 Ee BWANA, Mungu wetu, utuokoe,
Utukusanye kwa kututoa katika mataifa,
Tulishukuru jina lako takatifu,
Tuzifanyie shangwe sifa zako.
48Na ahimidiwe BWANA, Mungu wa Israeli,
Tangu milele hata milele.
Watu wote na waseme, Amina.
Haleluya.

Currently Selected:

Zab 106: SUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in