YouVersion Logo
Search Icon

Zaburi 129

129
Zaburi 129
Maombi Dhidi Ya Adui Za Israeli
Wimbo wa kwenda juu.
1 Wamenionea mno tangu ujana wangu;
Israeli na aseme sasa:
2 wamenionea mno tangu ujana wangu,
lakini bado hawajanishinda.
3 Wakulima wamelima mgongo wangu,
na kufanya mifereji yao mirefu.
4 Lakini Bwana ni mwenye haki;
amenifungua toka kamba za waovu.
5 Wale wote waichukiao Sayuni
na warudishwe nyuma kwa aibu.
6 Wawe kama majani juu ya paa,
ambayo hunyauka kabla hayajakua;
7 kwa hayo mvunaji hawezi kujaza vitanga vyake,
wala akusanyaye kujaza mikono yake.
8 Wale wapitao karibu na wasiseme,
“Baraka ya Bwana iwe juu yako;
tunakubariki katika jina la Bwana.”

Currently Selected:

Zaburi 129: NEN

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in