YouVersion Logo
Search Icon

Zaburi 112

112
Zaburi 112#112 Zaburi hii imetungwa kila mstari ukianzia na herufi ya alfabeti ya Kiebrania zikifuatana tangu Aleph (A) hadi Taw (T); zote ni 22.
Baraka Za Mwenye Haki
1 Msifuni Bwana.
Heri mtu yule amchaye Bwana,
mtu yule apendezwaye sana na amri zake.
2 Watoto wake watakuwa wenye uwezo katika nchi,
kizazi cha watu waadilifu kitabarikiwa.
3 Nyumbani mwake kuna mali na utajiri,
haki yake hudumu milele.
4 Hata gizani nuru humzukia mtu mwadilifu,
yule mwenye rehema, huruma na haki.
5 Mema yatamjia mtu yule aliye mkarimu na mwenye kukopesha bila riba,
anayefanya mambo yake kwa haki.
6 Hakika hatatikisika kamwe,
mtu mwenye haki atakumbukwa milele.
7 Hataogopa habari mbaya,
moyo wake ni thabiti, ukimtegemea Bwana.
8 Moyo wake ni salama, hatakuwa na hofu,
mwishoni ataona ushindi dhidi ya adui zake.
9 Ametawanya vipawa vyake kwa ukarimu akawapa maskini;
haki yake hudumu milele;
pembe yake itatukuzwa kwa heshima.
10 Mtu mwovu ataona na kuchukizwa,
atasaga meno yake na kutoweka,
kutamani kwa mtu mwovu kutaishia patupu.

Currently Selected:

Zaburi 112: NEN

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in