YouVersion Logo
Search Icon

Zaburi 111

111
Zaburi 111#111 Zaburi hii imetungwa kila mstari ukianzia na herufi ya alfabeti ya Kiebrania zikifuatana tangu Aleph (A) hadi Taw (T); zote ni 22.
Sifa Za Bwana Kwa Matendo Ya Ajabu
1 Msifuni Bwana.
Nitamtukuza Bwana kwa moyo wangu wote,
katika baraza la wanyofu na katika kusanyiko.
2 Kazi za Bwana ni kuu,
wote wanaopendezwa nazo huzitafakari.
3 Kazi zake zimejaa fahari na utukufu,
haki yake hudumu daima.
4 Amefanya maajabu yake yakumbukwe,
Bwana ni mwenye neema na huruma.
5 Huwapa chakula wale wanaomcha,
hulikumbuka agano lake milele.
6 Amewaonyesha watu wake uwezo wa kazi zake,
akiwapa nchi za mataifa mengine.
7 Kazi za mikono yake ni za uaminifu na haki,
mausia yake yote ni ya kuaminika.
8 Zinadumu milele na milele,
zikifanyika kwa uaminifu na unyofu.
9 Aliwapa watu wake ukombozi,
aliamuru agano lake milele:
jina lake ni takatifu na la kuogopwa.
10 Kumcha Bwana ndicho chanzo cha hekima,
wote wanaozifuata amri zake wana busara.
Sifa zake zadumu milele.

Currently Selected:

Zaburi 111: NEN

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in