YouVersion Logo
Search Icon

Zaburi 110

110
Zaburi 110
Bwana Na Mfalme Wake Mteule
Zaburi ya Daudi.
1 Bwana amwambia Bwana wangu:
“Keti mkono wangu wa kuume,
mpaka nitakapowafanya adui zako
kuwa mahali pa kuweka miguu yako.”
2 Bwana ataeneza fimbo yako ya utawala yenye nguvu kutoka Sayuni;
utatawala katikati ya adui zako.
3 Askari wako watajitolea kwa hiari
katika siku yako ya vita.
Ukiwa umevikwa fahari takatifu,
kutoka tumbo la mapambazuko
utapokea umande wa ujana wako.#110:3 Au: vijana wako watakujia kama umande.
4 Bwana ameapa,
naye hatabadilisha mawazo yake:
“Wewe ni kuhani milele,
kwa mfano wa Melkizedeki.”
5 Bwana yuko mkono wako wa kuume,
atawaponda wafalme siku ya ghadhabu yake.
6 Atawahukumu mataifa, akilundika mizoga
na kuwaponda watawala wa dunia nzima.
7 Atakunywa maji katika kijito kando ya njia,#110:7 Au: Yeye atoaye mtu wa kurithi mwingine atamweka kwenye mamlaka.
kwa hiyo atainua kichwa chake juu.

Currently Selected:

Zaburi 110: NEN

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in