Mpango wa kupigana Vita vya KirohoMfano
SIKU YA 3: Hofu ya kujisikia vibaya
Hofu ilianza kuendesha nafsi yangu nilipokuwa mtoto mdogo. Wazi kabisa nakumbuka kuiona roho ya hofu chumbani kwangu wakati wa usiku na kupiga kelele kumwita mama. Mama alikuja na mfagio na kuifukuza mbali, akiffikiria kwamba ilikuwa ni hisia zangu tuu zikifanya kazi. Lakini mara nyingi ilikuja tena na kisasi.
Nikiwa mkubwa, baada ya kuteseka na matukio mengi ya hofu, hofu ilitawala maisha yangu. Hofu ya kuogopa haikuwa tena hisia zangu. Nikuwa na jeshi la roho za hofu ambalo liliathiri kila eneo la maisha yangu na lilijidhihirisha katika njia nyingi.
Hofu ni mwarobaini wako. Ni silaha muhimu mkononi mwa adui ambayo inakataa ahadi za Mungu katika maisha yako. Hofu inakuja kusimamiaha katika maendeleo yako na Mungu. Lakini unaweza kuwa huru kutoka kwenye ngome yake katika akili yako. Unaweza kuchukua mamlaka dhidi yake inapojaribu kuinuka dhidi ya nafsi yako.
Baba, katika jina la Yesu nakuja kwako na kutubu kwa kuruhusu kujisikia hofu. Ninakemea roho ya hofu inayofanya kazi kunitega, kuiba imani yangu, amani yangu, na kunijaza na wasiwasi, katika jina la Yesu. Nachagua imani, tumaini, na upendo. Namcha na kumtumaini Bwana pekee, katika jina la Yesu. Amen.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Kwa haya mafundisho ya nguvu utaelewa kwa kina kuhusu jinsi ya kutengeneza njia ya kumpita adui na kuzuia mpango wake wa kuharibu maisha yako
More