Warumi 1Mfano
Injili ni Nguvu ya Mungu
Katika Warumi 1:16, Paulo anashiriki kuhusu uwezo wa Injili. Anasema ni uweza wa Mungu unaookoa mtu yeyote na kila aaminiye. Injili sio tu ujumbe wa Mungu katika kitabu cha zamani, Biblia. Injili ni ujumbe wenye nguvu. Ni uweza wenyewe wa Mungu uletao wokovu kwa wale wanaoamini. Injili inafanya kazi kwa nguvu kuleta wokovu kwa wale wanaoamini iwe Myahudi au Myunani. Injili inaweza kuokoa mtu yeyote na kila mtu si kwa sababu ya ushawishi wa mhubiri bali kwa sababu ya nguvu iliyobeba. Nguvu ya Mungu iokoayo.
Hii inatuambia kwamba wakati ujumbe wa Injili unashirikiwa sio tu kwamba tunasikia Mungu akisema lakini tunaweza kumtarajia kutenda. Injili inakuja na nguvu, uweza mkuu wa Mungu. Injili inafanya kazi kwa sababu Mungu anafanya kazi kwa nguvu kupitia kwayo. Injili inaweza kuokoa na kubadilisha mtu yeyote kwa sababu ni nguvu ya Mungu. Hii ina maana kwamba tunaposikia Injili, tunaposoma Biblia tunaweza kutarajia mabadiliko kutokea kwa sababu Mungu anatenda kazi. Inamaanisha pia tunapowaambia wengine Injili tunaweza kutarajia Mungu afanye kazi kwa uwezo wake. Tunaweza kupumzika katika faraja ya kujua kwamba Injili hufanya kazi daima kwa sababu Mungu hutenda kazi kupitia Injili.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Katika siku tano zijazo, tutachunguza Injili ni nini. Tutaona kuwa Injili ni ujumbe wa Mungu kutoka kwa Biblia na Yesu Kristo kwa watu wote, na ni nguvu ya Mungu kwa ajili ya wokovu.
More
Tungependa kumshukuru iServe Africa kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://utumishi.net/