Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Warumi 1Mfano

Warumi 1

SIKU 4 YA 5

Injili ni ya Watu Wote

Paulo anatuambia kwamba agizo la kuwaita watu kwa Yesu linatoka kwa Yesu mwenyewe na mapenzi yake ni watu wote kutoka mataifa yote waje kwake. Ujumbe wa Injili ni kwa ajili ya watu wote Wayahudi na Wamataifa. Wito wa Yesu ni kwa mataifa yote kuja na kuwa mali yake, kuja na kumtii. Moyo wake unalilia watu kutoka mataifa yote waje kwake wawe wake.

Yote hapa ina maana ya kila aina na aina ya watu, inamaanisha watu kutoka makabila yote, rangi na tabaka zote. Anawaita weupe kama anavyowaita weusi, wa kidini kama anavyowaita wasioamini na matajiri kama anavyofanya masikini. Wito wa Injili ni kwa watu wote. Watu wote wanahitaji kusikia ujumbe na wito wa Injili kumtii Yesu. Ni vizuri sana kujua kwamba sisi sote tunathaminiwa na Yesu. Kwamba bila kujali rangi au tabaka, Yesu anataka tuwe wake. Huu pia ndio ujasiri wetu tunaposhiriki ujumbe wa Injili ili kujua kwamba unawahusu wote.

Andiko

siku 3siku 5

Kuhusu Mpango huu

Warumi 1

Katika siku tano zijazo, tutachunguza Injili ni nini. Tutaona kuwa Injili ni ujumbe wa Mungu kutoka kwa Biblia na Yesu Kristo kwa watu wote, na ni nguvu ya Mungu kwa ajili ya wokovu.

More

Tungependa kumshukuru iServe Africa kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://utumishi.net/