Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Usionee Haya InjiliMfano

Usionee Haya Injili

SIKU 4 YA 4

Hubiri Injili

Katika utamaduni wetu wa Kiafrika, maneno ya baba anayeaga dunia ni muhimu kwa watoto wake. Kwa kawaida, maneno haya huthaminiwa kama maneno muhimu zaidi. Paulo anapokaribia mwisho wa huduma yake ya utume na anakabili kifo chake kinachokaribia, anaandika kile tunaweza kukiita maneno muhimu zaidi kwa mwana wake wa kiroho na kwetu.

"lihuubiri neno, uwe tayari wakati ukufaao na wakati usiokufaa," anaandika. Na sababu ya dharura hii ni ipi? Mstari wa 3 unajibu, "maana utakuja wakati watakapoyakataa mafundisho ya uzimai." Maelezo haya yanafaa kabisa kwa nyakati zetu—mafundisho ya ukweli na ya uzima hayapewi umuhimu leo. Watu wanapenda kujikusanyia walimu watakao waambia wanachotaka kusikia. Katika mazingira kama hayo, jukumu letu linabaki kuendelea kuhubiri injili, kuitangaza kazi ya Yesu msalabani kama habari njema pekee na yenye uzima.

Wale walio karibu nasi wanaweza kuwa wamepotelea katika mafundisho ya uwongo, labda kupitia makanisa wanayohudhuria au kupitia wahubiri maarufu katika vyombo vyetu vya habari. Kwa uvumilivu, tunaitwa kuwaeleza kuhusu Yesu na kuwaita kutoka kwenye mafundisho ya uwongo.

Andiko

siku 3

Kuhusu Mpango huu

Usionee Haya Injili

Tunaishi katika nyakati ambapo Injili ya kweli inaonekana kupoteza mvuto wake. Wengi hukimbilia kusikia yale yanayowapendeza, huku wachungaji wakijaribu kuifanya Injili ivutie zaidi. Kwa sababu hiyo, wengi wanaionea aibu Injili. Katika siku tano zijazo, tutatembea na Paulo kupitia 2 Timotheo, ambako anatuhimiza tusiionee aibu Injili, bali tuwe tayari kuteseka kwa ajili yake, kuilinda, kuendelea nayo, na kuihubiri.

More

Tungependa kumshukuru iServe Africa kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://utumishi.net/