Usionee Haya InjiliMfano
Endelea Ndani ya Injili
Paulo anarejelea siku hizi za mwisho kama nyakati za shida, hasa kwa sababu ya kuenea kwa walimu wa uongo. Walimu hawa wa uongo ni wapenda nafsi, wapenda pesa, wapenda anasa, na kila aina ya dhambi badala ya kuwa wapenda Mungu. Hawatachukia tu yaliyo kweli bali watapinga ukweli (2 Timotheo 3:1-8). Hata hivyo, sisi ambao tumemwamini Yesu na tunashikilia injili, tunaitwa tuendelee na ukweli huu (mstari wa 14).
Hakuna mtu anayekomaa kupita injili; hakuna hatua zaidi ya kuiendea. Tunapaswa kuendelea kushikilia mafundisho ya zamani ambayo yanatuongoza kwenye wokovu na kutuhifadhi hadi kuja kwa Bwana wetu. Kama inavyosemwa maarufu, “chochote kilicho kweli si kipya, na chochote kipya si kweli” Kutokuwa na aibu ya injili kunamaanisha kuendelea kuiamini, kuishikilia, na kuithamini ile injili ya kale and kweli, hata wakati kila mtu mwingine ameiacha.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Tunaishi katika nyakati ambapo Injili ya kweli inaonekana kupoteza mvuto wake. Wengi hukimbilia kusikia yale yanayowapendeza, huku wachungaji wakijaribu kuifanya Injili ivutie zaidi. Kwa sababu hiyo, wengi wanaionea aibu Injili. Katika siku tano zijazo, tutatembea na Paulo kupitia 2 Timotheo, ambako anatuhimiza tusiionee aibu Injili, bali tuwe tayari kuteseka kwa ajili yake, kuilinda, kuendelea nayo, na kuihubiri.
More
Tungependa kumshukuru iServe Africa kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://utumishi.net/