Baraka za Kiroho ndani ya ChristoMfano
Wakristo, tunao Muhuri wa Roho Mtakatifu
Wakati mtu anapomaliza kusoma, shule anayosomea humpa cheti cha kuonyesha kuwa amehitimu. Kwa kawaida, shule huweka Muhuri wao kwa cheti hiki ili kuthibitisha kuwa ni halali.
Sisi Wakristo waliopewa Urithi tuliopookolewa, Biblia inasema tumewekewa Muhuri na Roho Mtakatifu. Roho Mtakatifu ndiye anatuhakikishia ya kwamba tumeokolewa na tunao Urithi ndani ya Kristo. Roho mtakatifu hatuhimizi tu kuamini ili tuokolewa, lakini pia anatuhimiza kila siku tuishi maisha yanayo mpendeza Mungu tunapongoja kuja kwa Yesu. Yeye ndiye dhamana ya Urithi wetu mpaka kuja kwa Yesu, tutakapoupokea.
Roho Mtakatifu anapotuhimiza kuachana na dhambi na kutubu, hili ni hakikisho kuwa sisi tu Wakristo. Hivyo basi, tunafaa kuendelea kutii Roho Mtakatifu anapotuhimiza tuaachane na dhambi. Pia, tunafaa kushukuru Mungu kwa sababu Roho Mtakatatifu anatuhakikishia Urithi wetu ndani ya Kristo.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Je, unafikiri kwamba uko na kila baraka za kiroho ndani ya Kristo? Paulo akiwaandikia Waefeso anawaambia wamsifu Mungu kwa sababu amewabariki ndani ya Kristo. Ndani ya Kristo, hatuna tu baraka moja au mbili, ila tunazo baraka zote za kiroho.
More
Tungependa kumshukuru iServe Africa kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://utumishi.net/