Soma Biblia Kila Siku 10/2024Mfano
Sadaka inayompendeza Mungu na kukubaliwa naye ni kule kumtolea kwa hiari bila kulazimimishwa. Utoaji unaosimuliwa hapa ni ule wa kutengeneza hema ya kukutania. Nyumba ya Mungu na ufalme wake hujengwa na watu wenye moyo wa kupenda, watu wanaotii jinsi roho yao inavyowahimiza. Angalia kuwa kumtolea Mungu ni zaidi ya kumpa sehemu ya mapato, ni pia kuchangia kwa ustadi wako.Mfano mzuri umesimuliwa katika m.26:Wanawake wote ambao mioyo yao iliwahimiza katika hekima wakasokota hizo singa za mbuzi. Tunda la utoaji wa aina hiyo ni furaha na kuimarika kwa uhusiano wetu na Mungu. Mfano mmoja tunao katika 1 Nya 29:9:Watu wakafurahi, kwa sababu wametoa kwa hiari yao wenyewe, kwa sababu kwa ukamilifu wa moyo, kwa hiari yao wenyewe, wamemtolea Bwana; mfalme Daudi naye akafurahi kwa furaha kuu. Na Paulo anakumbusha hivi katika 2 Kor 9:7:Kila mtu na atende kama alivyokusudia moyoni mwake, si kwa huzuni, wala si kwa lazima; maana Mungu humpenda yeye atoaye kwa moyo wa ukunjufu.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 10/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Kumi pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Waebrania, Kutoka na 2 Wafalme. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz