Soma Biblia Kila Siku 08/2024Mfano
“Utauwa” ni maisha ya uchaji wa Mungu. Hufaa kwa mambo yote. Kwa hiyo neno la leo linatuambiakujizoezakuupata. Tufanyeje? Mazoezi ya mwili, fikra na nia hayatatufanikisha. Kwa hiyo Timotheo anaambiwa kujiendeleza kiroho kwa njia ya kuwamzoevuwa maneno ya imani na mafundisho mazuri ya Biblia:Uwakumbushe ndugu mambo hayo, nawe utakuwa mtumishi mwema wa Kristo Yesu, na mzoevu wa maneno ya imani, na mafundisho mazuri yale uliyoyafuata(m.6). Hivyo tunamwekeaMungutumaini letu, alivyofanya Paulo. Tafakari anavyoshuhudia katika m.10:Twajitaabisha na kujitahidi kwa kusudi hili, kwa sababu tunamtumaini Mungu aliye hai, aliye Mwokozi wa watu wote, hasa wa waaminio. Mungu ndiyeMwokozi wa watu wote, kwa sababu hayupo Mwokozi mwingine, nahasa wa waaminio, kwa sababu ni hao tu watakaookolewa.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 08/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Nane pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha 2 Wafalme na 1 Timotheo. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz