Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Silaha za Mungu - Matendo ya MitumeMfano

Silaha za Mungu - Matendo ya Mitume

SIKU 4 YA 10

Mshipi wa Ukweli

HADITHI YA BIBLIA – Anania na Safira Matendo 5:1-10

Sehemu ya kwanza ya Silaha iliyotajwa katika Waefeso sura ya 6 ni mshipi wa ukweli, kifaa ambacho kinafungwa kiunoni na askari na kusaidia kushikilia pamoja Silaha nzima. Mshipi unashikilia Silaha katika mwili wa askari, unashikilia upanga mahali pake, na ni kifaa ambacho askari hawezi kuondoa. Kwa kweli, ikiwa askari hana mshipi wa ukweli, labda hata mavazi yake yataanguka chini, na kuaibika mbele ya kila mtu! Sehemu moja ya ukweli ni mambo tunayosema na vinywa vyetu. Tunapaswa kuwa Wakristo ambao husema ukweli tu, sio kusema uwongo kwa wazazi wetu au kwa Mungu. Lakini sehemu nyingine ya mshipi wa ukweli ni kwamba tunachagua kumwamini Mungu na Neno Lake. Ukweli ni kwamba adui yetu, Ibilisi, kila wakati anajaribu kusema uwongo na kutudanganya kwa kuamini vitu ambavyo sio vya kweli.

Katika hadithi ya leo ya Bibilia, Anania na Safira waliamini uwongo kwamba haikuwa muhimu kuwa waaminifu mbele ya wanafunzi. Walijifanya kuwa wameuza mali zao kwa pesa kidogo kuliko zile walizopata. Waliamini adui ambaye aliwafanya wadhani kwamba Mungu hangewaona au hakujua maelezo ya mauzo. Lakini Mungu huona kila kitu. Wanafunzi walikuwa wawakilishi tu wa Mungu. Na kwa sababu walisema uwongo mbele ya wanafunzi, hivyo walisema uwongo mbele ya Mungu. Walificha ukweli kuhusu mauzo yao kwa sababu waliamini uwongo ambao shetani aliwafanya waamini. Je, ni uongo gani unaoamini ambao unaweza kusababisha Silaha yako ianguke?

Ni muhimu kwamba kila wakati tuvae mshipi wa ukweli kwa kusema ukweli kila wakati na kwa kuamini ukweli kuhusu Mungu na Neno lake kila wakati.

"Nachagua kuishi kwa uaminifu."

MASWALI :

1. Ikiwa wewe sio mwaminifu, nini kinafanyikia mshipi wako wa kweli? Je, hili litaathiri sehemu zingine za Silaha yako?

2. Je, ni hali gani ambapo husemi 'uongo' lakini unakosa 'uaminifu'?

3. Matokeo ya uwongo ni gani?

4. Anania na Safira wote waliwezaje kusimulia hadithi inayolingana kuhusu mauzo ya mali zao ingawa kulikuwa na muda wa saa tatu walipongumza na Petro?

5. Anania na Safira walimwambia nani uwongo?

siku 3siku 5

Kuhusu Mpango huu

Silaha za Mungu - Matendo ya Mitume

Kuvaa Vazi la Kivita la Mungu sio ibada ya maombi ya kufanya kila asubuhi lakini mtindo wa maisha tunaoweza kuanza tukiwa wadogo. Mpango huu wa kusoma ulioandikwa na Kristi Krauss unawaangazia mashujaa kutoka katika kitabu cha Matendo ya Mitume.

More

Tungependa kumshukuru Equip & Grow kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.childrenareimportant.com/swahili/armor/