Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Silaha za Mungu - Matendo ya MitumeMfano

Silaha za Mungu - Matendo ya Mitume

SIKU 1 YA 10

Ulimwengu Usioonekana

Hadithi Ya Biblia – Yesu apaa mbinguni " Matendo 1:1-11 "

Kuna ulimwengu usioonekana karibu nasi na upo kihalisia, ingawa hatuwezi kuuona. Kama tu jinsi hauwezi kuona upepo, lakini unaweza kuona jinsi miti inavyosonga wakati upepo unavuma kupitia majani, ndivyo ilivyo katika ulimwengu wa kiroho. Mmoja wa manabii wa Agano la Kale, Elisha, anatoa mfano mzuri wa kuona ulimwengu huu usioonekana. Kuna vita vinavyokaribia kuanza kati ya Aramu na Israeli. (2 Wafalme 6: 8-23)

Usiku mmoja, askari wa maadui walizunguka jiji, na wakati mtumishi wa Elisha alipowaona, aliogopa sana. Lakini nabii akamwambia mtumishi wake asiogope kwani kulikuwa na askari zaidi katika upande wao kuliko upande wa adui. Ndipo Elisha akaomba ili macho ya mtumishi wake yafunguliwe, alipotazama aliona vilima vilivyojaa farasi na magari ya moto yakiwazunguka! Mungu alikuwa na jeshi kubwa lisiloonekana lililomlinda nabii wake!

Kuna vita vya kiroho vinavyotuzunguka, ingawa hatuwezi kuviona. Bibilia inaweka wazi kuwa Shetani yuko na anajaribu kutufanya tupuuze ukweli wa ufalme wa kiroho. Katika hadithi ya leo ya Bibilia kutoka kitabu cha Matendo, tunaona Yesu akipaa mbinguni. Tafadhali niamini, mbingu na kuzimu zipo. Katika hadithi hii ya kihistoria, baada ya Yesu kupaa, malaika wawili walijitokeza kwa wanafunzi! Ni vigumu kuwaza malaika wakija ili kutusaidia au shetani akitushambulia, lakini vitu hivi vipo kihalisia. Wacha tuangazie somo hili kuhusu Silaha ya Mungu na tujifunze zaidi kuhusu ulimwengu huu usioonekana.

Tuko kwenye vita, iwe tunaitikia au tunapuuza.Kwa hivyo, hebu tuvalie Silaha kamili ya Mungu tunapopigana na adui!

"Ninachagua kuamini katika ulimwengu huu usioonekana na kuvaa Silaha kamili ya Mungu."

Maswali

1. Je, una ushahidi wowote kuhusu ulimwengu usioonekana wa mema na mabaya?

2. Je, umeshuhudia wengine ambao wametenda makosa na hawaonekani kulindwa na Silaha ya Mungu?

3. Je, unadhani vita vya kiroho vinavyotuzunguka vinakaaje?

4. Je, ni nani aliyetoa ahadi kwamba Yesu atarudi kwa njia ile ile aliyoondoka?

5. Jaza nafasi tupu zinazotoka katika kitabu cha Matendo 1:8: Mtakuwa mashahidi wangu katika

…__________________________________________. Je, maneno haya yana maana gani kwetu sasa?

siku 2

Kuhusu Mpango huu

Silaha za Mungu - Matendo ya Mitume

Kuvaa Vazi la Kivita la Mungu sio ibada ya maombi ya kufanya kila asubuhi lakini mtindo wa maisha tunaoweza kuanza tukiwa wadogo. Mpango huu wa kusoma ulioandikwa na Kristi Krauss unawaangazia mashujaa kutoka katika kitabu cha Matendo ya Mitume.

More

Tungependa kumshukuru Equip & Grow kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.childrenareimportant.com/swahili/armor/