Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Soma Biblia Kila Siku /Septemba 2023Mfano

Soma Biblia Kila Siku /Septemba 2023

SIKU 4 YA 30

Vyombo vya ghadhabu(m.22) ni Waisraeli. Hao ni taifa teule waliotendewa kila tendo jema na Mungu, lakini wakawa na mioyo migumu ,wakazifuata njia zao wenyewe. Mungu aliwavumilia sana! Kwa uamuzi wake hata Mwana wake akazaliwa katika taifa hili! Lakini wakamwua!Vyombo vya rehema(m.23) ni watu wa Mataifa waliomwamini Yesu (m.25-26:Ni kama vile alivyosema katika Hosea, Nitawaita watu wangu wale wasiokuwa watu wangu, Na mpenzi wangu yeye asiyekuwa mpenzi wangu. Tena itakuwa mahali pale walipoambiwa, Ninyi si watu wangu, Hapo wataitwa wana wa Mungu aliye hai) - pamoja na Waisraeli wachache (m.27:mabaki; m.29:uzao). Rudia m.30:Tuseme nini, basi? Ya kwamba watu wa Mataifa, wasioifuata haki, walipata haki; lakini ni ile haki iliyo ya imani. Hivyo Mungu ametufunulia ghadhabu yake, uweza wake na utukufu wake.Ni nini basi, ikiwa Mungu kwa kutaka kuonyesha ghadhabu yake, na kuudhihirisha uweza wake, kwa uvumilivu mwingi, alichukuliana na vile vyombo vya ghadhabu vilivyofanywa tayari kwa uharibifu;tena, ili audhihirishe wingi wa utukufu wake katika vile vyombo vya rehema, alivyovitengeneza tangu zamani vipate utukufu(m.22-23)!

siku 3siku 5

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku /Septemba 2023

Soma Biblia Kila Siku /Septemba 2023 ni mpango mzuri wa kusoma biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa septemba pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi k...

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha