Soma Biblia Kila Siku/AGOSTI 2023Mfano
Yesu akisema, ”Mimi niko” (m.58), anajitambulisha kama Mungu. Ni sawa na ilivyo katika Kut 3:14 ambapoMungu akamwambia Musa, MIMI NIKO AMBAYE NIKO; akasema, ndivyo utakavyowaambia wana wa Israeli; MIMI NIKO amenituma kwenu. Wayahudi walitambua hiyo, lakini kwa kuwa walitumia ufahamu wa kibinadamu tu kuhusu historia waliyoifahamu juu ya Yesu, walikataa kumwamini. Hata wakamshtaki kwamba ni mtu mbaya (Msamaria) mwenye pepo, na kutaka kumpiga mawe kwa sababu ya kumkufuru Mungu. Badala ya kulipokea neno la Yesu kwa imani wasionje mauti, sasa wakabaki katika hatari ya kufa katika dhambi zao kwa sababu hawakumwamini. Hiyo Yesu aliwaambia wazi:Mtakufa katika dhambi zenu; kwa sababu msiposadiki ya kuwa mimi ndiye, mtakufa katika dhambi zenu(m.24). Wewe je, unamwamini Yesu kuwa Mungu?
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Agosti 2023 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kuelewa somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu Yohana na Mithali. Karibu kujiunga na mpango huu.
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/