Soma Biblia Kila Siku/AGOSTI 2023Mfano
Ni ajabu uponyaji wa Yesu ulivyo! Angalia jinsi kusudi la kuja kwake linavyotimia kwa njia hiyo:Yesu akasema, Mimi nimekuja ulimwenguni humu kwa hukumu, ili wao wasioona waone, nao wanaoona wawe vipofu(m.39).Mara moja maneno ya uzima yanatiririka kutoka katika moyo wa kipofu aliyeponywa mwili kuonyesha kuwa ameponywa roho pia. Hata anageuka na kuwa mwalimu wa viongozi wa kidini, kama tunavyosoma katika m.30-33:Yule mtu akajibu, akawaambia,Hii ni ajabu! Kwamba ninyi hamjui atokako, naye alinifumbua macho! Twajua ya kuwa Mungu hawasikii wenye dhambi; bali mtu akiwa ni mcha Mungu, na kuyafanya mapenzi yake, humsikia huyo. Tokea hapo haijasikiwa ya kuwa mtu ameyafumbua macho ya kipofu, ambaye alizaliwa hali hiyo. Kama huyo asingalitoka kwa Mungu, asingeweza kutenda neno lo lote(m.30-33). Bali kwa upande wa hao, upofu wao wa kiroho unazidi tu kwa sababu hawapokei uponyaji wa Yesu unavyomshuhudia kwamba ametoka kwa Mungu. Uchaguzi mzuri kwetu ni kumwamini Yesu ili kuponywa upofu wetu.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Agosti 2023 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kuelewa somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu Yohana na Mithali. Karibu kujiunga na mpango huu.
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/