Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Kumwakisi YesuMfano

Kumwakisi Yesu

SIKU 3 YA 3

Neno wosia linamaanisha “agano.” Kwa hiyo unaposoma Wosia mpya basi, unasoma kuhusu agano jipya. Yesu alipokuwa akijiandaa kufa msalabani, alishiriki mlo wa mwisho pamoja na wanafunzi wake. Ulikuwa ni mlo wa Pasaka, lakini Yesu aliupa umuhimu mpya (Luka 22:14 – 20). Katika mlo huo, alisema, “Kikombe hiki ni agano jipya lililothibitishwa kwa damu yangu; inayomwagika kwa ajili yenu” (Aya 20).

Kwa agano hili jipya yaja baraka ya pekee sana imeandamana nayo. Tunasoma kuhusu hilo katika Waebrania: “Vivyo hivyo Yesu amekuwa dhamana ya agano lililo bora zaidi… Kwa hiyo aweza sikuzote kuwaokoa wale wanaomjia Mungu kwa yeye, kwa kuwa yu hai sikuzote ili kuwaombea” (Ebr. 7: 22,25).

Yesu alipokuwa duniani, misheni yake— “maelezo ya kazi yake”—ilikuwa ni kutimiza sheria na kulipia dhambi zetu msalabani. Sehemu ya maelezo ya kazi yake sasa katika agano jipya ni kufanya maombezi kwa ajili ya watakatifu, ambayo inajumuisha wewe (9:24; 10:19 – 22). Haupo peke yako. Hauko pweke.

Yesu sasa anakufanya maombezi kwa niaba yako. Lakini njia pekee ya kupata uzoefu wa uwezo wake wa kuokoa kila siku ni kwa kujifungamanisha naye kwa kujiweka chini yake. Unapofanya hivyo, unapata baraka za utunzaji Wake.

Kupata uzoefu wa baraka hizi yajumuisha kuwa na uwezo wa kufurahia kibali cha Mungu katika maisha yako mwenyewe na kueneza kibali chake Mungu kuwafikia wengine. Sisi si “Wakristo wasio kwenda popote.” Sisi ni mifereji. Mungu kamwe hakukusudia baraka zake ziende umbali usiozidi zaidi ya maisha yetu wenyewe. Anatamani sisi tuwe mifereji ambayo kwayo baraka zake zitatolewa kwa wengine.

Yesu alikuja ili tuwe na uzima na tuwe nao tele (Yohana 10:10). Alianzisha kanisa lake kama mwili wake mwenyewe, ambao yeye ndiye kichwa chake. Kama mwili wake, tumeitwa kutumikiana. Kupendana mmoja na mwingine, Kuheshimiana sisi kwa sisi, kutiana moyo mmoja na mwingine, kusamehe mmoja na mwingine, elekezana mmoja na mwingine. Kimsingi, tunapaswa kumwakisi na kumheshimu Yesu katika maneno na matendo yetu sisi kwa sisi.

Uhusiano wetu wa wima na Mungu—urafiki wetu na Yeye na ufikiaji wetu kwa mamlaka na baraka zake—unafungamanishwa na uhusiano wetu wa mlalo na mwili wake ambao ni, kanisa. Katika uhusiano wetu na watu wengine, inaweza kusemwa kwamba sisi ni "Yesu mlalo" kwa wengine. Kwa sababu Kristo yu ndani yetu, wengine wanapaswa kumwona Yesu ndani yetu. Yeye ndiye kichwa chetu na sisi—kanisa lake, familia yake ya waumini—ni mwili wake, tunaoishi chini ya ubwana wake.

Ikiwa unamjua mtu anayeugua ugonjwa wa kutetemeka, unajua, kuna kule kutengana ambako hutokea kati ya kile ambacho ubongo huashiria na kile ambacho mwili hufanya. Misukumo ya neva inayothibiti mwondoko huacha kufanya kazi vyema. Hii inafadhaisha sana kwa mtu binafsi, kwa sababu mwili umeundwa kufuata ishara kutoka kwa kichwa.

Ndivyo ilivyo kwa mwili wa Kristo. Tunapaswa kufanya kazi kikamilifu chini ya uongozi wa kichwa chetu, Kristo. Tunapaswa kumwakisi Yesu katika yote tunayofanya. Sisi ni mikono na miguu yake.

Tunatamani wengine watutendee kwa heshima, na Yesu anataka vivyo hivyo kutoka kwetu. Kumheshimu katika yote tunayofanya huleta upendeleo wake.

Je, unawezaje kumheshimu Yesu kwa mawazo, maneno, na matendo yako? Hapa kuna baadhi ya mapendekezo:

  • Mawazo: Jiulize: Je, mawazo yangu yanamheshimu Bwana au ninajishughulisha na nafsi yangu tu?
  • Maneno: Ifanye iwe mazoea ya kumwonyesha Yesu heshima kupitia maneno yako unayozungumza na wengine kwa heshima wanayostahili kama watu walioumbwa kwa mfano wake.
  • Vitendo: Weka shajara kwa wiki moja ya jinsi unavyotumia wakati wako. Baada ya kuhakiki shajara yako, chunguza uone kama unamheshimu na kumwakisi Yesu kwa nafasi ya kwanza maishani mwako.

Maisha na huduma ya Yesu haina mwisho. Yuko katika mahali pake palipoinuka mbinguni ... na yuko ndani yako. Acha maisha na huduma yake yatiririke kutoka kwako unapomwakisi yeye katika kile unachofikiri, kufanya na kusema.

Tunatumai kuwa mpango huu umekuhimiza. Ili ujue zaid kuhusu huduma ya Tony Evans, bofya hapa.

siku 2

Kuhusu Mpango huu

Kumwakisi Yesu

Maisha ya Yesu hapa duniani iliisha na upeo mkubwa: Ufufuo wake, kuonekana baada ya ufufuo, na kupaa mbinguni kimwili. Lakini umewahi kujiuliza nini kilitokea baadaye? Yesu anafanya nini siku hizi? Katika kitabu hiki cha Waefesim Tony Evans anatumia mpango huu mfupi wa usomaji, kutupa kuona kidogo tu jukumu la Yesu sasa na jinsi tunavyopaswa kumwakisi Yeye katika maisha yetu ya kila siku.

More

Tungependa kuwashukuru The Urban Alternative (Tony Evans) kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: Home - The Urban Alternative