Kumwakisi YesuMfano
Ninapenda krimu katika kahawa yangu. Sijawahi kunywa kahawa yangu ikiwa nyeusi. Wakati wowote ninapomwaga kahawa katika kikombe, mimi huongeza krimu nyeupe na kuchanganya pamoja. Wakati huo, muungano huwa umetokea. Wakati mmoja nilikuwa na kahawa nyeusi na krimu nyeupe, lakini sasa nina kahawa ya kahawia. Ikiwa nitachukua kahawa pamoja nami katika ofisi yangu, krimu inakuja pia. Ikiwa nitachukua krimu pamoja nami kwenye pango langu, kahawa inakuja pia. Hakuna kinachoweza kuwatenganisha wawili hawa mara tu wameunganishwa.
Yesu Kristo analeta pamoja vitu vyote mbinguni na duniani. Mapenzi ya Mungu ni “kuleta kila kitu pamoja katika Masihi.” Paulo alisema hivi katika Kitabu cha Wakolosai: “Yeye amekuwako kabla ya vitu vyote, na vitu vyote hushikana katika yeye” (Kol. 1:17).
Ninapohubiri mara nyingi narudia mambo ili kusisitiza jambo fulani. Wazazi mara nyingi hufanya vivyo hivyo na watoto wao. Paulo alifanya hivyo katika Waefeso 1.
“... ndani Yake…” (Aya 7)
“... ndani Yake ...” (Aya wa 9)
“... ndani ya Masihi ...” (Aya 10)
“... ndani Yake.” (Aya wa 10)
Ndani Yake, yeye pekee ambaye ametukuka wala hakuna mwingine kama yeye, utagundua ukamilifu na muhtasari wa kila kitu utakachohitaji mbinguni na duniani. Yote yamo…. ndani Yake. Kila kitu unachohitaji kwa maisha ya ushindi wakipata ndani ya Yesu.
Mara nyingi tunapoteza nguvu na mamlaka ya Yesu kwa sababu hatukai ndani yake. Wakolosai 1:13 inatuambia kwamba Mungu “alituokoa kutoka katika milki ya giza na kutuhamisha na kutuingiza katika ufalme wa Mwana anayempenda.” Ulikuwa raia wa ufalme wa Shetani, lakini sasa, kama muumini, wewe ni sehemu ya ufalme mpya, na Yesu Kristo ndiye Mfalme wake. Shetani hawezi kufanya lolote ili kukuondoa katika ufalme wa Mungu, lakini atafanya yote awezayo kukufanya upuuze utawala wa ufalme wa Yesu Kristo.
Je, hii inawezaje kutokea katika maisha ya Mkristo? Inatokea tunaposhiriki kanisani Jumapili chini ya ufalme mmoja, lakini jumatatu hadi jumamosi twakwenda ulimwenguni na kufanya kazi chini ya ushawishi wa ufalme mwingine. Hii inatokea tunapojifunza Biblia katika ufalme mmoja, lakini tunafanya ujamaa katika ufalme mwingine. Waumini wengi hujihusisha katika kuyapindua maisha yao kwa ghafula, huku na huko, kisha hushangaa kwa nini hawana ushindi katika maisha yao.
Shetani anashawishi maisha ya waaminio kwa sababu wanakabidhi uwezo wao kwake; si kwa sababu ya mamlaka yoyote halali aliyonayo, bali kwa sababu tu ya wao kushindwa kufungamanisha mawazo na maamuzi yao chini ya ubwana wa Yesu Kristo. Kwa kutomwinua Yesu Kristo mahali panapofaa katika maisha yetu, nyumbani, na makanisa—mahali pa kwanza anapostahili—tunakosa manufaa ya kufunikiwa na yeye.
Je, unataka manufaa anayotoa kwa watu wake? Basi kaa ndani yake na umwakisi yeye katika yote ufanyayo.
Kuhusu Mpango huu
Maisha ya Yesu hapa duniani iliisha na upeo mkubwa: Ufufuo wake, kuonekana baada ya ufufuo, na kupaa mbinguni kimwili. Lakini umewahi kujiuliza nini kilitokea baadaye? Yesu anafanya nini siku hizi? Katika kitabu hiki cha Waefesim Tony Evans anatumia mpango huu mfupi wa usomaji, kutupa kuona kidogo tu jukumu la Yesu sasa na jinsi tunavyopaswa kumwakisi Yeye katika maisha yetu ya kila siku.
More
Tungependa kuwashukuru The Urban Alternative (Tony Evans) kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: Home - The Urban Alternative