Kumchukua Mungu Kwa UzitoMfano
Katika soka, kila kitu kinapimwa kulingana na eneo la mpira. Mpira huendelezwa kuchezwa tokea mahali hapo ulipo wekwa chini kwanza. Kugusa na kuweka mpira chini, inategemea iwapo mpira ulivuka mstari ulioko nyuma ya goli la mpinzani. Goli la uwanja linahesabiwawakati mpira unapita kati ya nguzo mbili. Kila kitu kinapimwa kwa uwepo wa mpira. Ukweli huo ndio huamua kila kitu kinachotokea kwenye mchezo, haswa matokeo ya mchezo.
Vile vile, uhusiano wako na agano utaamua kina cha uhusiano wako na Mungu, au uhusiano huo utakuwa juu juu kiasi gani. Itaamua ni umbali gani na kasi gani unasonga mbele maishani. Itaamua ikiwa utafunga mabao au ikiwa itabidi uendelee kupiga tu mpira kwa kujihifadhi. Muhimu zaidi, itaamua kiwango chako cha mafanikio - ikiwa utashinda au utapoteza. Kiwango chako cha mafanikio kimeungamanishwa na uhusiano wako na agano.
Huenda umemkubali Yesu Kristo kama Mwokozi wako binafsi, na unaweza kuwa umefanyika mtoto wa Mfalme kupitia kuzaliwa upya katika roho. Lakini kama hujaunganishwa kwa njia ya uhusiano wa agano, huwezi kupata uzoefu kamili wa mipango yake kwa ajili yako. Mafanikio ya kiroho yanapatikana kupitia muunganisho uitwao utakaso, sio tu kupitia kuhesabiwa haki kisheria.
Je tofauti gani iliyoko kati ya kuokolewa na kutakaswa?
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Kwa sababu tumepata upendo na neema nyingi za Mungu, ni rahisi kuwa mlegevu kuhusu utii. Hatumchukulii Mungu kwa uzito vya kutosha. Tunaacha kumcha na hatuzingatii matokeo ya kutotii kwetu. Mruhusu mwandishi Tony Evans aambaye vitabu vyake vyauzwa sana akufundishe kuhusu baraka zinazotokana na kuweka agano na Mungu na hatari inayotokea tunapoacha kumchukulia kwa uzito.
More
Tungependa kuwashukuru The Urban Alternative (Tony Evans) kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: Home - The Urban Alternative