Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Siku Saba Za Kufanya Sala Wakati Upitiapo MajonziMfano

Siku Saba Za Kufanya Sala Wakati Upitiapo Majonzi

SIKU 4 YA 7

Vaa Viatu vya Amani

Hebu tuombe,

“Baba, ninavaa viatu vya amani huku nikikabiliana na kero la huzuni ya kile nilichopoteza. Tuliza maji yangu yaliyochafuka, Bwana. Acha nitembee juu ya bahari inayochafuka na viatu vya amani. Sema nami, ee Bwana, maneno haya: “Amani, tulia!” [Marko 4:39]. Acha nione uwepo wako kama shalom moyoni mwangu, Mungu. Dhoruba katika moyo wangu ninaihisi mithili ya dhoruba kali kwenye bahari. Ninanena shalom katika moyo wangu, katika akili yangu, na katika hisia zangu. Ninanena shalom kwa miguu yangu na katika matendo yangu. Acha amani inizuie kuongeza maumivu zaidi na hasara zaidi kwa hali hii kwa kusema au kufanya jambo lisilo la busara. Katika jina la Kristo, amina.”

Andiko

siku 3siku 5

Kuhusu Mpango huu

Siku Saba Za Kufanya Sala Wakati Upitiapo Majonzi

Siku 7 za Sala zimeundwa kwa minajili ya kuimarisha roho yako na kuhimiza moyo wako wakati upitiapo majonzi. Kila siku inajumuisha sala utakayofanya wewe au kutumia kama msingi wa maombi yako kuhusu mada ya siku hiyo ili kupata nafuu kutokana na majonzi. Katika siku hizi 7 utapata tumaini kutoka kwenye Neno la Mungu na kutiwa moyo kwa kujua kwamba upendo wake na faraja ni zako katika hali yoyote.

More

Tungependa kuwashukuru The Urban Alternative (Tony Evans) kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: Home - The Urban Alternative