Siku Saba Za Kufanya Sala Wakati Upitiapo MajonziMfano
Vaa Mshipi wa Ukweli
Hebu tuombe:
“Baba, katika hasara yangu, najisikia kutokuwa na utulivu na mwenye kutikisika. Ninaomba kwamba utanitegemeza ninapojifunga mshipi wa ukweli. Asante kwa kuwa nami hata katika giza totoro ya huzuni yangu. Bwana, naomba adui asipate nafasi kupitia hasara haribifu iliyonikumba. Mungu, tafadhali nisaidie ili hasara hii isije ikajenga ndani yangu mzizi wa uchungu ambao Shetani anaweza kuutumia kunielekeza kwenye njia isiyo sawa. Sitaki hasara hii, Bwana, lakini sina budi kutumaini kwamba Wewe ni Mungu mwema ambaye huchagua na kuruhusu yale yaliyo bora kwangu, hata katika hili. Katika jina la Kristo, amina.”
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Siku 7 za Sala zimeundwa kwa minajili ya kuimarisha roho yako na kuhimiza moyo wako wakati upitiapo majonzi. Kila siku inajumuisha sala utakayofanya wewe au kutumia kama msingi wa maombi yako kuhusu mada ya siku hiyo ili kupata nafuu kutokana na majonzi. Katika siku hizi 7 utapata tumaini kutoka kwenye Neno la Mungu na kutiwa moyo kwa kujua kwamba upendo wake na faraja ni zako katika hali yoyote.
More
Tungependa kuwashukuru The Urban Alternative (Tony Evans) kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: Home - The Urban Alternative