Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maombi Ya Kusudi Katika Ndoa YakoMfano

Maombi Ya Kusudi Katika Ndoa Yako

SIKU 6 YA 6

Upanga Wa Roho

"Kuna baadhi ya wake ambao hupokea zawadi ya kumbukumbu kila mwaka. Mume wao anarudi nyumbani kutoka kazini, anampeleka mke wake kwa chakula cha jioni, anampa zawadi nzuri, na kufanya mambo mengi ya kuifanya siku hii kuwa ya kipekee na yenye umuhimu mkubwa. Lakini ndivyo hivyo. Mke hasikii tena kutoka kwake kwa njia za upendo, na shukrani kwa mwaka mzima. Lakini anajua kwamba mwaka ujao kwenye maadhimisho yao, kutakuwa na zawadi nyingine nzuri, wakati wa pamoja mzuri na maneno ya upole. Je, unadhani wake hao wameridhika na uhusiano huo? Au unafikiri kwamba wangefurahia kubadili hiyo siku moja ya ukumbusho wa kila mwaka ili wawe na siku 364 mfululizo kwa mwaka ambazo zilikuwa za uaminifu na thabiti na zilizojaa mawasiliano? Hata hivyo ndivyo wengi wetu tunafanya na Mungu.” Tony Evans.

Bwana, kutumia muda pamoja, mmoja na mwingine kama wanandoa ni kipaumbele na inapaswa kuwa kipaumbele katika ndoa yetu. Lakini kutumia muda na wewe katika Neno lako katika uwepo wako ni muhimu kwa kuwa na ndoa yenye ushindi, hasa kwa kuwa inahusiana na sisi kutimiza kusudi ulilotupatia. Tusaidie, Baba, kulifanya kuwa jambo la kwanza kukaa ndani yako na Neno lako. Tusaidie kufanya hivi kama wanandoa lakini pia kama watu binafsi. Hatutaki kujihusisha sana na familia, shughuli na hata katika kukutumikia wewe na kila mmoja wetu hata kusahau umuhimu wa kutulia mbele yako na kulifanya Neno lako kuwa kitu tunachotumia wakati mwingi na kwa mara kwa mara.

Unasema wazi kwamba tukikaa ndani yako na neno lako, tunaweza kuomba chochote tunachotaka na utafanya. Utatufikisha kwenye kituo tulichokusudia na kuturidhisha sisi kama wanandoa katika kutimiza makusudi yetu binafsi na vile vile makusudi yetu ya pamoja. Ufunguo wa kuishi kusudi letu unapatikana katika kukaa ndani yako na Neno lako.

Neno lako ndilo litakaloshinda vita vyetu—ni upanga wa Roho ambao utabatilisha uongo wa adui unaotufanya tuwe na hamu ya kuacha kufuata mpango wako. Neno lako ni upanga wa Roho, utakaotupatia hekima ya kujiepusha na vinavyo tuvuruga vya miili yetu wenyewe. Tusaidie kutenga muda katika Neno lako liwe jambo tunalofanya mara kwa mara kuliko tunavyofanya sasa. Tuonyeshe njia za ubunifu za kufanya hivi, na tunakushukuru mapema kwa kusikia na kujibu maombi haya. Katika jina la Kristo, amina.

Tunatumahi kuwa mpango huu ulikuhimiza. Kwa habari zaidi kuhusu wizara, bofya hapa.

Andiko

siku 5

Kuhusu Mpango huu

Maombi Ya Kusudi Katika Ndoa Yako

Kamwe katika historia ya ulimwengu taasisi ya ndoa haijawahi kuwa chini ya chunguzi kama ilivyo. Kila siku, jamii hutafuta kufafanua upya maana ya kuoa, na Wakristo wanakabiliwa na ukosoaji mkubwa zaidi kwa kushikilia kile kinachoitwa mtazamo na wa mawazo finyu kuhusu ndoa. Kwa hivyo kusudi la kibiblia la ndoa ni nini, na tunapaswa kuombaje kama waumini ili kuhifadhi maana yake? Katika kampeni yetu ya siku sita, Maombi ya Kusudi katika Ndoa Yako, wanandoa wanaweza kuomba kuwepo na maana katika ndoa yao wenyewe, na pia kuthibitisha ufahamu wa kimungu wa muungano wa agano kati ya mwanamume na mwanamke.

More

Tungependa kuwashukuru The Urban Alternative (Tony Evans) kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://tonyevans.org/